Michel Platini kukaa pembeni ya wadhifa wa uraisi wa UEFA
baada ya kupunguziwa adhabu yake toka miaka 6 hadi miaka 4 na mahakama ya soka
CAS.
Platini aliadhibiwa
na kamati ya nidhamu ya FIFA miaka 8 kutokana na malipo ya euro million 1.3
aliyopokea kutoka kwa raisi wa FIFA Sepp Blatter mwaka 2011.
Imedaiwa kuwa fedha
hizo zilikuwa kwa ajili ya malipo ya kazi aliyoifanya kwa Blatter mwaka
1998-2002. Adhabu yake ya miaka 8 ilipunguzwa hadi miaka 6 na kamati ya rufani
ya FIFA.
Platini alitumaini
kusafishwa na shutuma zote lakini watu watatu kutoka CAS walirudisha hukumu ya
FIFA ya kuwa malipo hayakuridhisha na ni mgongano wa kimaslahi.
Hata hivyo upande
huo uliongeza kuwa adhabu hiyo ya kusimamishwa kwa miaka 6 ni kubwa na
ikapunguzwa hadi miaka 4.
Katika maelezo
yake Plaatini alisema utawala ni kama kutoelewa na ni kinyume cha sheria na
kuendelea kupambana kusafisha jina lake kupitia mfumo wa sharia wa Uswiss.
Mwanasheria wa
Platini amethibitisha kuwa atajiuzulu kama raisi wa UEFA siku chache zijazo.
Mahakama imesema
kuwa Platini amepokea fedha zaidi ya miaka 8 kufikia mwisho wa mahusiano ya
kazi yao, haikuegemea katika nyaraka yoyote ambayo imeanzishwa kwa wakati huo
wa mahusiano ya kimkataba na hakumualika na kutoridhika sehemu ya pesa yake
isiyolipwa.
Post a Comment