Kwa mujibu wa kituo cha redio cha Capital FM jijini Nairobi, mmoja wa
waliokabiliwa na polisi alifariki baadaye akipokea matibabu.
"Kikosi
cha Polisi ni kikosi cha nidhamu na si kikosi cha kutumia nguvu. Kanuni
ziko wazi kuhusu jinsi ya kuwashughulikia raia wakati wa maandamanaji,”
tume hiyo imesema kupitia Twitter.
Mamlaka huru ya kiraia
inayofuatilia shughuli za polisi (IPOA) pia imeshutumu vitendo vya
maafisa wa polisi na kusema walivuka mipaka.
Mwenyekiti wa mamlaka hiyo Bw Macharia Njeru amewaambia wanahabari kwamba polisi walitumia nguvu kupita kiasi.
Amesema
maafisa wa mamlaka hiyo wanakamilisha uchunguzi na watawasilisha ripoti
kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) ili hatua zichukuliwe dhidi ya
maafisa husika.
Muungano wa upinzani CORD umekuwa ukifanya maandamano Jumatatu kila
wiki kuwashinikiza maafisa wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC)
wajiuzulu.
Viongozi wa CORD wamesema maafisa hao hawawezi kusimamia uchaguzi huru na wa haki wakati wa uchaguzi mkuu ujao 2017.
Wameahidi kuendelea na maandamano hayo hadi maafisa hao watakapong’atuka.
Post a Comment