MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekipongeza kituo cha redio cha EFM kwa kuanzisha shindano lijulikanalo kama ‘Shika ndinga na EFM’, lenye lengo la kuwasaidia wananchi wa hali ya chini na kati katika kujikwamua na umaskini.
Akizungumza hivi karibuni wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano hilo, Makonda alisema shindano hilo ni zuri na linamanufaa kwa wananchi kwani halina chembe ya wizi bali ni nguvu na akili ya mtu ndo uhitajika ili kuweza kushinda.
“Naishukuru sana EFM kwa kuanzisha shindano hili kwani nilivyoliona si la wizi ni shindano ambalo linamtaka mshiriki kutumia akili yake na nguvu zake ili kuweza kushinda, hivyo basi nawaomba wananchi washiriki katika mambo ambayo yanamanufaa kwao na si yale yanayowapotezea muda,” alisema Makonda.
Hata hivyo Makonda amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea kuzingatia suala la usafi na kutambua kuwa usafi ni jambo la muhimu katika maisha ya kila siku.
Fainali ya shinda ndinga na EFM wamefikia tamati na kupatikana kwa washindi wawili waliojishindia gari aina ya Keri mahususi kwa kubebea mizigo.
Post a Comment