Baada ya taarifa nyingi kutolewa kuhusu hukumu ya mpenzi wa zamani wa Msanii wa bongo fleva Ney wa Mitego Siwema Edson wakili wa kesi hiyo Moris Mtoi amejitokeza na kuongea ukweli kuhusu ukweli wa hukumu hiyo.
Mtoi alisema kuwa Siwema alihukumiwa kwa kosa la kutafuta mali kwa kwa njia ya vitisho ambapo siwema alimtishia mpenzi wake mpya kuwa atasambaza picha za utupu walizopiga na mpenzi wake mpya endapo hatomnunulia baadhi ya mali alizozitaka.
Baada ya vitisho hivyo mpenzi wa siwema aliamua kumnunulia gari aina Honda CRV ambalo halikupunguza ukali wa lengo la Siwema kwa aliendela kudai ajengewe nyumba na kupewa pesa taslim.
Siwema alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mnamo tarehe 21 April 2016 baada ya mpenzi wake huyo kufikisha kesi mahakamani mnamo April 2016.
Aidha Mtoi amekanusha uvumi wa kesi iliyokuwa ikimkabiri Siwema kuwa si ya matusi mitandaoni bali ni kutafuta mabi kwa njia ya vitishio.
SOURCE MILLARD AYO
Post a Comment