Halloween party ideas 2015
Image


Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Dudu Baya amechukizwa na tabia za baadhi ya wasanii wa muziki ambao husaidiwa na label zao na baadae kuondoka kwa maneno ya kashfa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dudu Baya amesema kitendo alichokifanya Mo Music cha kuondoka kwenye label iliyomtoa kisa haijamfia video sio cha kiungawana.
“Swala la wasanii wa bongofleva kuvunja ndoa zao na record lebal wanazofunga nazo ndoa ni sugu na niendelevu. Tatizo katika hili nila wasanii. Wanaingia mikataba ili tu kwanza wapate umaarufu kasha watoke, Wakishaupata umaarufu huo, huwa wanageuka na kuona maslahi kwao ni madogo, ndio maana huwa wanaanza migomo ili waongezewe maslahi kinyume na mkataba,” alisema Dudu.
Aliongeza, “ Wasanii wengi wa bongo wamekuwa waongo sana na utumia nafasi ya kuwadanganya mashabiki wao pindi wapatapo airtime ya kufanya interview redioni au kwenye runinga, nawaomba mashabiki muwapuuze wasanii wanaowadanganya,”
Mo Music ameachana na menegement yake ambayo imemtoa kimuziki kwa madai imeshindwa kumtimizia baadhi ya mambo kwa wakati.


Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.