Na Yusuph Mwamba
Mkuu wa mkoa wa dar es salaam akizindua mradi wa ujenzi wa viwanda vidogo vidogo mwananyamala dar es salaam.
RC makonda ameweka jiwe la msingi may katika viwanda vidogo vidogo katika karakana ya jiji iliyopo mwananyamala dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amezitaka Manispaa zote za Mkoa wake zitengeneze mazingira rafiki kwa wajasiriamali wadogo ili iwe rahisi kujiwezesha.
RC Makonda amesema kwa kufanya hivyo itawarahisishia wao kuwa tambua kwa urahisi pindi watakapojiunga kwenye vikundi ili kujipatia mikopo itakayo wasaidia kuongeza nguvu katika biashara zao.
Akizungumza mara baadaya kuweka jiwe la msingi katika uzinduzi wa viwanda vidogovidogo katika Karakana ya Jiji iliyopo Mwananyamala Jijini Dar es Salaam.
"Ni wapongeze kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa manispaa lakini pia kuunga mkono jitihada za wajasiriamali kwa kuwapa mikopo kupitia vikundi vyao na nitoe wito pia kwa watendaji msitoe mikopo holela itakuwa kazi kuzirejesha". Alisema RC
Amewapongeza Halmashauri ya Jiji kwa kuanza kutoa Ruzuku kwa manispaa kwani hapo mwanzo walikuwa hawatoi.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo wa ujenzi viwanda vidogo vidogo kwa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam SIPORA LIANA amesema kuwa kupitia mradi huo Jiji la Dar es Salaam limeendelea kutoa kipaumbele kwa wanawake, vijana na walemavu wanaopata mikopo kutoka Halmashauri ya Jiji kwakuwa mazingira wanayofanyia kazi sio rafiki na wanahangaika sana kupata masoko.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonlin
Post a Comment