Na Yusuph Mwamba
KIKAO cha kwanza cha mikakati ya mipango kazi dhidi ya rushwa na utwala bora kimefunguliwa leo rasmi na Naibu Mkurugenzi mkuu wa Takukuru ,Bregedia Jenerali John Mbungo kwenye ukumbi wa Anatogro Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Generali Mbungo amesema kuwa lengo la mpango huo ni kuhakikisha Taifa linaondokana na rushwa ili kuhakikisha sera ya Viwanda inakamilika.
Aidha, Generali Mbungo, amesema kuwa huu ni mpango wa tatu, ukiachilia mbali na mipango miwili iliyopita ambapo mpango wa kwanza ulizinduliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu mnamo tarehe 10, Desemba, 2016.
Utekelezaji huo wa kikao kazi cha kudhibiti uadilifu mkoa wa Dar es salaam ulianza tarehe 1 Julai, 2017 utekelezwa.
Pia amesem serikali inatarajia miradi ya maendeleo inatatekelezwa kwa wakati kutokana na thamani ya fedha iliyotengwa kwenye miradi hiyo.
Akifafanua kuhusu utendaji wao, wamejikita haswa katika kudhibiti rushwa ikiwemo sekta ya madini, nishati, mafuta ya gesi pamoja na hakiza za binadmu na mengineyo.
Serikali imeunda kamati za kuratibu mikakati kuanzia ngazi za mikoa na wilaya kwa ajili ya kuziongezea nguvu kamati ya mpango wa tatu wa sasa.
Moingoni mwa kazi za mkakati wa kudhibiti rushwa na utawala bora awamu ya tatu ni pamooja na kuandaa mipango kazi katika utekelezaji wa majukumu husika na kusiamia mipango kazi hiyo.
Wageni walihudhuria katika uzinduzi huo wa kikao kazi cha wajumbe wa kudhibiti uadilifu mkoa wa Dar es salaam ni pamoja na Juventus Baitu mkuu wa Takukuru kanda maalumu ya Dar es salaam, Christina Maganga mratibu wa kitengo cha utawala bora , Theresia mmbando katibu tawala mkoa wa Dar es salaam na wadau mbali mbali.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonlin
Post a Comment