WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania kutolalamika kwa uamuzi wowote unaofanywa na serikali ya sasa, kwani una nia njema kwa mustakabali wa Taifa.
Mwigulu amewataka Watanzania kuendelea
kumwombea Rais John Magufuli ambaye anadhihirisha kwa vitendo kuchukia
wizi na ufisadi ili nia njema aliyonayo kwa taifa, aifikie. Akitoa
salamu katika ibada ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Luis, Dar es Salaam jana,
Mwigulu alisema kuna uamuzi Serikali inaochukua huenda usieleweke kwa
haraka lakini una lengo jema kwa taifa.
Alitoa mfano kuwa Rais Magufuli
anachukia kwa vitendo rushwa na ufisadi hivyo hawezi kucheka wakati
akifanya uamuzi, kwa kuwa hakuna dini yoyote inayomchekea shetani wakati
wa kumkemea. “Ili nchi ipige hatua kuna mambo yalikuwa lazima
yafanyike. Kuna mambo si rahisi kuyaelewa kwa haraka haraka, lakini
niwasihi mwendelee kumwombea rais kwa kuwa ana nia njema.
“Mkimwombea Rais na sisi tunapata lifti
humo humo na mambo yanaenda,” alisema Mwigulu. Alisema uovu ni lazima
ukemewe na kutolea mfano Yesu Kristo alipoingia hekaluni na kukuta
biashara inafanyika, alipindua meza na kufungulia njiwa kwa ukali na
ndivyo anavyofanya Rais. “Mmeshawahi kuona shetani anakemewa kwa upole?
Uovu lazima ukemewe kwa nguvu,” alisema Mwigulu.
Kuhusu kuchangia ujenzi wa kanisa hilo,
Mwigulu alisema ni muhimu kuchangia ujenzi wa nyumba za ibada kwa kuwa
zinapunguza uovu katika jamii. Alisema mikoa yenye nyumba nyingi za
ibada, uovu nao unapungua na ikiwa watu hawatajitoa kuchangia Mungu,
huruhusu wapate hasara ili ifidie uchoyo waliouonesha kumwibia Mungu.
Kanisa hilo la Usharika wa Mbezi Luis linajengwa kutokana na bomoabomoa
inayoendelea katika barabara ya Morogoro .
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline .
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline .
Post a Comment