Na Mwandishi wetu
JAMHURI Kihwelo
‘Julio’ ambaye ni mnazi mkubwa wa Simba, amesema mabeki wa Yanga, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani, watashangaza wadau siku ya mechi ya
Ngao ya Jamii, Agosti 23, itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
“Simba, wasije
wakajibweteka wakidhani, beki ya Yanga ni mbovu, ninachokiona ni kocha George
Lwandamina, anakiandaa kikosi chake, kujifunga dhidi ya Ruvu, siyo sababu hayo
ni maandalizi tu, wapo kina Cannavaro na Yondani, wana uwezo wa juu na
wazoefu.
“Huwezi kukibeza
kikosi cha Yanga, wakati kipo kwenye maandalizi kwa sababu kocha anakuwa
anampima kila mchezaji ili kujua ubora na madhaifu yake, kujifunga ni
mambo ya kawaida na hilo atalifanyia marekebisho ndani ya siku 10
zilizosalia,”alisema kocha huyo wa Dodoma FC.
Julio alisema
Simba , ndiyo ipo kwenye hatari zaidi tofauti na majina makubwa wanayoyaamini
mashabiki kwa maana ya kikosi ni kipya kinatakiwa kukaa kwa pamoja kwa
muda mrefu, ili kutengeneza kombinesheni ya wachezaji.
“Simba ni timu mpya, kocha
atakuwa na kazi ngumu kuliko Yanga, ambao wengi ni wazamani wameongezeka
wachache, wageni, wajipange vilivyo kuendana na uhalisia wa uwanjani na si
kishabiki,”alisema Julio ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba.
MSIKIE CANNAVARO
Naye nahodha wa
Yanga, Cannavaro, alisema anaiamini beki yao kwani kujifunga dhidi ya Ruvu ni
jambo la kawaida akitolea mfano kwamba hata Ulaya, inatokea “Ni kawaida na ujue
haya ni maandalizi siyo kwamba tupo kwenye ligi.”
“Kocha anampa nafasi
kila mchezaji, kujua anaweza akafiti wapi ni mapema sana kujaji mtu kwa sasa,
ila kuhusu Ngao ya Jamii, tumejipanga na tunacheza mechi za kirafiki kujiweka
sawa,”alisema mchezaji huyo mzoefu.
Kwa upande wa katibu
mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alizungumzia maandalizi kwa ujumla kwamba
yanaenda vizuri, wakitambua kwamba ni mechi ya ushindani wa hali ya juu, ila
matarajio yao ni ushindi.
‘Tupo kwa ajili ya
kushindana naamini tutafanikiwa kushinda mechi hiyo, najua Simba wanajipanga
ila watakutana na muziki mnene wa wachezaji wa Yanga, kama kiongozi naona
maandalizi yapo imara,”alisema
Emmanuel Martin ni
straika wa timu hiyo, alisema kufungwa na Ruvu inasaidia kujifunza na kujua
mapema mapungufu yapo wapi “Simba wakidhani kwa sababu Yanga, walijifunga na
Ruvu ni mbovu, basi tutakutana Agosti 23, pale taifa ndipo watajua tupo
vipi,”alisema.
Yanga, wamecheza
mechi mbili za kirafiki jijini Dar es Salaam, dhidi ya Singada United na
kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, Uwanja wa Uhuru, huku
wakijifunga bao 1-0, dhidi ya Ruvu Shooting ya Masau Bwile, Uwanja wa
Chamazi.
KOTEI ACHEKELEA
Kiungo wa Simba,
Mghana James Kotei amezinasa kuwa beki wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’
amejifunga mwenyewe kwenye mechi ya kirafiki, akacheka na kumwonea huruma,
lakini akasisitiza kwenye mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi yao, watawachapa
mengi tu.
Kotei amesema:
“Ninachokiamini kwa Simba yetu hii, mbali na kushinda, Yanga tutawafunga mabao
mengi tu na tuna kila sababu ya kufanya hivyo. Ukiangalia timu yao
kuanzia beki, kiungo na ushambuliaji, tunawazi.”
“Tena kwa beki yao
ile. Nimesikia mechi ya kirafiki waliyocheza beki kajifunga, ni huruma
naona linapokukuta hili ni shida, lakini jambo kama hili watu wanatakiwa
kuelewa inatokea tu,”alisema Kotei.
IUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline .
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline .
Post a Comment