Halloween party ideas 2015
Image


Na Yusuph Mwamba
ASSALAM ALAIKUM Kwanza niwatakie kheri ya mwezi mtukuf wa Ramadhan rafiki zangu wote.
Kichwa cha habari ya makala hii nimekinukuu kutoka kwa sheikh aliyehutubu katika msikiti wa Ijumaa mjini Tanga, pia maudhui ya habari yenyewe nimeyapata kutoka kwa sheikh huyu maaruf Sheikh Kakhtwan ni Naibu Mudir wa Taasisi ya Ansaar Muslim.

Nitafurahi zaidi kuona watu baada ya kusoma makala hii wakai - share ili waislam wote wafaidike na waadhi huu kupitia mtandao wa facebook, na Haya ndio matumizi mazuri ya mtandao ambayo Mungu ataturidhia.

Sheikh ameeleza mambo mengi ambayo yanafanya swaum zetu pengine zisiwe ni zenye kukubaliwa na Mungu Lakini nimenukuu nukta kadhaa ambazo nimeiona ni lazima nanyi mzipate.

1. KUFUNGA BILA YA KUSWALI.

waislamu wengi wanaipa heshma ibada ya funga na kuitelekeza swala, hili ni kosa kubwa kwa mfungaji na huenda funga yake ikawa ya mashaka. Hivyo basi mwenye kufunga ni lazima aswali vipindi vyote vitano.

2. KUFUNGA BILA YA UKARIMU
Kadhalika waislam wengi hufunga Lakini nafsi zao hazibadiliki na kuwa ni wenye huruma na imani kwa waislam wenzako, umefunga Lakini hujali kama kuna waislamu wenzako hawana futari. Hili nalo ni kosa.

3. KUFUNGA KULA NA KUNYWA TU.
waislam wengi hufunga kwa kuacha Kula na kunywa Lakini Bado huendelea na matendo ya maaswi kama kawaida. Mfano kusema uongo, kusengenya, kuiba, kudhulumu, kuzini baada ya ftari na kadhalika.

matendo hayo hayafai siku zote Lakini hayafai zaidi ikiwa umefunga hapo ni Sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

4. KUFUNGA BILA YA KUIJUA RAMADHAN
Waislamu wengi imegundulika wanafunga bila ya kuwa na ilmubya mwezi mtukufu wa Ramadhan, yaani kwanini tunafunga, faida za funga ni Zipi kidini na kiafya, nini hasara za mwenye kuacha kufunga, ni yapi yafanyike kipindi cha mwezi wa Ramadhan na ni yapi hayafai kuyafanya japo ni halali.
Sheikh akatoa mfano wa maswali yanayojirudia katika madarasa na yanaulizwa na watu wazima ambao wamefunga ramadhan zaidi ya Ishirini. Mtu anauliza "inafaa kumuingilia mkeo ukiwa umefunga?" Haya ni mambo ya kujifunza Tangu Ramadhan za mwanzo.

Hivyo ni Muhimu kuwa na Ilmu ya mwezi wa Ramadhan kama vile huwezi kutengeneza gari mpaka ukae Kigali.upfundishwe namna ya kutengeneza gari. Na ujuzi mwingine wowote....

5. KUFUNGA BILA YA KUSOMA QURAN.
Waislamu wengi hufunga Lakini husahau kusoma Kitabu kitakatifu - Quran Kareem, tumesahau au hatujui kuwa Quran imeshushwa ndani ya mwezi huu mtukufu. Na kuisoma ndani ya mwezi huu kuna fadhila nyingi zaidi kuliko Ile miezi mingine. 

Sheikh ameeleza hapo zamani watu wachaMungu walikuwa wakisoma Quran na kuikamilisha ndani ya siku tatu.

Lakini kwa sasa watu wanakosa Hata ukurasa mmoja, hii ni kuisahau Quran hivyo sheikh amesisitiza tusome Quran japo juzuu moja kwa siku na mwezi ukiisha tutakuwa tumekamilisha msahafu mzima.

6. KUFUNGA BILA YA KUMUIGA MTUME
Waislam wengi wanafunga kwa kuwaiga wazazi wao au jamii iliyowazunguka, itakuwa ni Sawa kama wao wanamuiga mtume Lkn itakuwa si Sawa kama wanafunga bila yakujua mtume ilikuwa ni silo summa zake wakati wa Ramadhan. 

Sheikh akatoa mfano Mtume (SAW) alipokuwa akifungua funga yake yaani kufturu alifuturu kwa Kula tende au kunywa maji na hii ins faida upande wa afya. Ni wakati gani mtume alikula Daku, wengi wetu hula daku saa nne au tano Usiku, mtume hakufanya hivyo.
Hivyo ni muhimu Kuiga funga ya mtume.

7. KUFUNGA HUKU UNAPOTEZA MUDA KWA MICHEZO NA KULALA.

Waislam wengi imekuwa ni ada kwao kufunga huku muda mwingi wakiutumia kulala au kucheza michezo kama karata, drafti, dhumna, keram na kadhalika. 


Hakika hii ni hasara kubwa tuliyonayo. Muislam anafunga anaamka saa sita mchana anaoga anaingia msikitini anaswali dhuhuri watu wakibaki msikitini kusoma Quran yeye anatoka anakwenda maskani kupiga soga na.kucheza michezo tofauti. Na hasara iliyoje mambo Haya kufanywa na watu wazima. Hivyo waislam tunakumbushwa kuepukana na mambo Haya ya kulala sana na kufanya mchezo mwezi huu wa Ramadhani.

8. KUFUNGA BILA YA KUJALI KUKUBALIWA KWA IBADA HII.
Waislam wengi hufunga kwa mazoea na hawana wasiwasi kuwa ibada hii imekubaliwa na Mungu au la! Ni kweli huwezi kujua wala hatuwezi kujua kama ibada zetu za funga zimekubaliwa, lakini ili kujiwekea mazingira ya kukubaliwa ni lazima kuwa na ghofu na wasiwasi kwa kila jambo ambalo tunafanya na ukiwa na wasiwasi nalo ni bora kuuliza au kuacha.

9. KUFUNGA KWA KUPANGA RATIBA ZA KULA KULIKO IBADA.
Waislamu ifikapo mwezi wa Ramadhani hurundika vyakula majumbani na kukaa na familia zao na kuongea watu wale nini iftari na daku watakula nini, lakini hakuna anayethubutu kuitisha kikao na family yake na kuongea kuhusu mpangilio wa ibada, watu wasome juzuu ngapi kwa siku waamke saa ngapi kufanya qiyamu llayli.

Akina mama wamekuwa wakishughulishwa majumbani kupika sana kiasi Hata wanakosa muda wa kusoma Quran kusikiza Darasa iwe misikitini au kwenye radio.




JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, 
insta@wabunifumediaonline

.



Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.