Na Yusuph Mwamba
MKURUGENZI Mgodi wa dhahabu wa Geita GGM uliopo Mkoani Geita, Richard Jordinson amesema kuwa wametoa jumla ya shilingi milioni sabini kwaajili ya kugharimia ujenzi wa bomba la maji taka lililoko kwenye Gereza kuu la Wilayani humo..
MKURUGENZI Mgodi wa dhahabu wa Geita GGM uliopo Mkoani Geita, Richard Jordinson kulia akizungumza na waandishi wa habari jana wakti wa mkutano wake wakutaka kusaidia ujenzi wa bomba la magereza |
Ameyasema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika mjini Geita ambapo ameongeza kuwa walipata maombi kutoka kwa mkuu wa mkoa huo na mkuu wa wilaya hiyo.
“Tulipokea maombi ya kuombwa kusaidia vifaa vya ujenzi kwenye Gereza la wilaya kutokana na kwamba sisi pia ni jamii na siku zote tunapenda kuona jamii inayotunzunguka inanufaika na uwepo wetu”amesema Jordinson.
Hata hivyo, kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo, Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga ameushukuru mgodi huo huku akisisitiza ujenzi kufanyika kwa weledi zaidi.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment