Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
BARAZA  la wazee barani Afrika limelaani kitendo cha rais wa Marekani, Donald Trump cha kuiondoa nchi yake katika makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi yenye lengo la kuikoa dunia na uharibifu wa mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa baraza la wazee barani Afrika na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Koffi Annan amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni tisho kubwa kwa kipindi hiki hivyo makubaliano ya Paris ni matokeo ya makubaliano mengi ya ushirikiano na utashi wa kutafuta suluhu ya pamoja ya tatizo la dunia.
Hakuna nchi moja inayoweza kuvuruga makubaliano yetu. wakati Marekani inajiondoa inadhoofisha na kunyong,onyeza mkataba huu wa kimataifa, lakini bado nchi nyingi zimesimamia msimamo wa pamoja,”amesema Annan.
Hata hivyo, ameongeza kuwa kilicho baki kwa sasa katika mkataba huo wa Paris ni kuongeza juhudi za kutatua matatizao ya mabadiliko ya tabia ya nchi ilikuweza kuikoa dunia na tatizo hilo.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, 
insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.