·
Wanawake
wanusurika kubakwa, watoto kumezwa na chatu
Na Yusuph Mwamba, WM
BAADHI ya wakazi wa mtaa wa Mgeule Juu, Kata ya Buyuni manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam wametishia
kutoshiriki uchaguzi mkuu ujao kwa kukosa huduma muhimu ya maji.
Wakazi hao walitoa kauli hiyo
hivi karibuni wakati wakizungumza
na waandishi wa habari waliokuwa kwenye ziara ya kihabari ya kutembelea
maendeleo ya jamii katika maeneo ya
pembezoni mwa manispaa hiyo.
Mmoja wakazi hao Zaituni Hassan alisema wamekuwa wakilazimika kunywa
maji yasiyokuwa salama katika maisha yao yote tangu ya eneo hilo likiwa kijiji
kabla ya Ilala kupandishwa hadhi kuwa Manispaa na vijiji kuwa mitaa.
“Kuna haja gani ya kuchagua viongozi kama kila wakati tunashiriki
chaguzi, kuahidiwa na kila anayekuja kuomba kura lakini wanapochaguliwa
wanaondoka na hawageuki nyuma?,”alihoji.
Akifafanua, Hassan alisema wanawake na watoto wamekuwa wakinusurika
kubakwa, kujeruhiwa na nyoka huku watoto
wakiokolewa kutoka kwenye midomo ya chatu wakati wakitafuta maji kwenye
chemichemi za kinyeji zilizochimbwa na wanamtaa kwenye mabonde na vichaka
vinavyozunguka eneo hilo.
Mkazi mwingine, Salumu Tupa alisema wamekuwa wakinywa maji ya chumvi
au kulazimika kununua maji yasiyokuwa na madini hayo kwa Shilingi 500 kwa ndoo
au dumu moja la lita 20 kutoka kwa wachuuzi.
“Hata hayo ya chumvi, unapofika wakati wa kiangazi hukauka hivyo tunazimika kwenda kwenye chemichemi za kienyeji, kununua kwa bei kubwa zaidi. Je mtu mwenye familia kubwa ataweza kumudu kununua maji na kumudu huduma nyingine za kifamilia?, “alihoji Tupa.
Alisema hali hiyo imechengia kuzorota kwa maendeleo miongoni mwao hasa
wenye kipato kidogo kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta maji na kuacha
kujielekeza kwenye shughuli zingine za uzalishaji mali.
“Sisi ni binadamu, tunahaki ya kupata maji safi na salama, maji
tunayokunywa ni kama wanyama, hatuna sababu ya kushiriki chaguzi zijazo kama
hali hii itaendelea,”alisisitiza.
Mjumbe wa kamati ya maendeleo
ya mtaa huo, Baraka Koka alikiri eneo hilo kukabiliwa ta tatizo la miundombinu
chakavu ya barabara, ukosefu wa daraja linalounganisha eneo hilo na maeneo
mengine ya jiji wakati wa msimu wa mvua,
maji safi na salama, soko, shule, umeme na zahanati.
Alisema baadhi ya changamoto zimefikishwa serikalini ingawa juhudi za
makusudi za kumaliza changamoto hizo kupitia
wawakilishi wa wananchi Bungeni na Baraza la Maendeleo la Manispaa.
“Kwa hiyo ni sahihi kusema yatosha kuchagua viongozi ambao
tunawachagua kila wakati wa uchaguzi kwa ahadi ya kumaliza kero lakini hakuna
anayegeuka nyuma, sasa tusema basi!,”alisisitiza Koka.
Akizungumzia kadhia hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala (DC), Sophia Mjema
alisema kuwa Wilaya yake imo kwenye mpango wa kuanisha maeneo yote yenye kero zilizokithiri ili kuingizwa katika
bajeti ya 2017/2018 .
Alisema wananchi wanapaswa kuwa na subra wakati serikali inapoainisha
maeneo hayo na kusisitiza kwamba hakuna eneo ambalo litaachwa.
“Wawe wavumilivu, hivi tunavyozungumza Mkurugenzi wa Manispaa na timu
yake wako kazini katika hatua za uanishaji huo hasa maeneo ya pembezoni mwa
Manispaa ikiwamo eneo hilo,”alisema DC Mjema.
Hivi
karibuni timu ya waandishi wa habari wa taasisi ya habari ya Wabunifu (WM) na
ile la Waandishi wa Habari za Uwazi na Uchunguzi, Sauti ya Wasiokuwa na Sauti Vijijini
(TTAJA) walifanya ziara katika mtaa huo na kushuhudia maji yenye rangi ya maziwa kutumika katika
shughuli mbalimbali na wananchi hao ikiwamo kunywaJIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment