Na Tatu Muhamed
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa hakuna sababu ya taasisi za Serikali kushindwa kulipa bili ya maji wakati taasisi hizo zinapewa fedha kutokana serikalini ikiwa watu wenye hali ya chini wanalipa.
Aidha Prof. Kitila, amesema kazi kubwa inayotakiwa kufanyika kwasasa ni kuhakikisha miradi yote inamalizika kwa haraka ili wahitaji wa maji waweze kuhudumiwa bila matatizo yoyote.
Profesa Mkumbo, ameyasema hayo jana katika ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya maji, ambapo pamoja na mambo mengine aliipongeza Dawasco kwa kazi kubwa wanayoifanya kwani ukilinganisha na huko nyuma ambapo malalamiko ya maji yamepungaua kwa kiasi kikubwa.
Prof. Mkumbo amesema haiwezikani mwananchi wa kawaida anamudu kulipa bili ya maji halafu taasisi za serikali ambazo zinapewa fedha zinashindwa kulipa hivyo lazima wahakikishe wanalipa na Dawasco wanatakiwa wafanye kazi hiyo ya kukusanya bili hizo za maji.
‘’Nawapongeza Dawasco kwani mnafanya kazi kubwa binafsi nimekuwa nikiwafuatilia hata kabla sijaingia wizarani kwakweli mnafanya kazi kubwa na mnastahli kupongezwa lakini muendelee hivyo na kwakweli wananchi wanataka maji si vinginevyo, " amesema Mkumbo na kuongeza kuwa:
"Wananchi wa kawaida wenye kipato cha chini wanalipa iweje kuwe na Taasisi ambazo hazilipi?. Ni lazima walipe, Rais aliposema Taasisi zisizolipa umeme zikatiwe, hakumaanisha umeme pekee.... Tunahitaji pesa kuwekeza kwenye miundombinu na Taasisi zote zinabajeti za kulipa bili, kwahiyo zilipe, " amesema Prof Mkumbo.
Aidha Prof. Mkumbo, amesema pamoja na kazi kubwa katika kufanikisha swala la maji linakuwa historia, amesema kuwa watoke kwenye lengo badala yake wahakikishe tatizo la maji linakwisha kabla ya kufika 2020 kwani kuna miradi mikubwa mno ya maji ambayo inatekelezwa na kama ikikamilika basi shida ya maji itakuwa imepata suluhisho.
Mkumbo aliongeza kuwa lazima shirika litoke kwenye mtazamo na kuingia kwenye uhalisia na hiyo ndiyo kazi kubwa iliyopo na hapo nikuona watu wanapata maji huku kibainisha maeneo kama Bonyokwa,Pugu,Chanyanyikeni Kinyerezi, maeneo hayo kwa kiasi kikubwa yanakabiliwa na Changamoto kubwa ya maji na yeye kama Katibu amepongeza Dawasco kwa kuliona hilo.
Pro. Mkumbo, amesema ni aibu kuona katika kipindi cha miaka 50 bado kuna tatizo la maji hivyo lazima wakimbie mbio na huo ndio utakuwa ugomvi wake mkubwa kwa watendaji na atahakikisha anawasumbua mno lakini lengo kuona wananchi wanapata maji.
Awali akitoa uwasilishaji wake kwa katibu huyo Ofisa Mtendaji mkuu wa Dawasco Sypriani Luhemeja, Prof. Mkumbo, amesema kuwa shirika hilo limepiga hatua kubwa ukilinganishana na huko nyuma ambapo uzalishaji ulikuwa chini.
Alisema hivi sasa Dawasco wanazalisha lita milioni 480 kwa siku na hitaji ni milioni 512 nakudai kuwa kiwango hicho ni kikubwa ukilinganisha na huko nyuma na kwamba bado wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba wanamaliza tatizo la maji katika mkoa wa Dar es Salaama na Pwani.
Aidha amefafanua kuwa uzalishaji wa maji katika ruvu chini ni lita milioni 217 ,ruvu juu lita mil, 196 na kutoka mtoni lita 9000 na vyazo vinginevyo vinachangia kwa asilimi ndogo huku akibainisha kuwa jumla ya wateja 187,087 wamehudumiwa na lengo nikuwafikia wateja 400000, ifikapo mwezi juni 2017.
Akizungumzia Changamoto za shirika hilo, Luhemeja amesema ni usambazaji wa maji pamoja na upotevu wa maji ambapo katika kipindi cha mwaka 2015 maji yalipotea kwa asilimia 57 na kufikia mwezi machi mwaka huu maji yamepotea kwa asilimia 37.8.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment