Na Issa Ramadhani
MADEREVA wa magari ya kubeba mafuta wanatarajiwa kugoma nchini Nigeria.
Wanachama wa mojawapo ya vyama viwili vikuu vya biashara ya mafuta wanalalamika kuhusu malipo duni na hali mbaya ya barabara nchini.Mgomo huo wa muda usiojulikana unatishia kuwaathiri mamilioni ya watu iwapo makubaliano hayatofikiwa
Madereva wa magari hayo ya mafuta ambao ni wanachama wa chama cha wafanyakazi wa mafuta na gesi Nigeria - wanalalamika kuhusu hali duni za utendaji kazi.
Mgomo huo ulitangazwa wiki iliopita baada ya chama cha wafanyakazi na serikali kushindwa kufikia makubaliano.
Ukosefu wa mafuta ni jambo la kawaida Nigeria.
Mwaka jana mzozo kuhusu bei ya mafuta ulisababisha msongamano na misururu mirefu katika vituo vya kuuza mafuta kwa wiki kadhaa
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment