Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba 
POLISI  mjini Washington nchini Marekani, wamemfyatulia risasi mwanamke mmoja aliyekuwa ndani ya gari, baada ya yeye kugonga gari la polisi karibu na bunge la Marekani na baadaye kujaribu kuwagonga maafisa kadha wa polisi.
Mwanamke huyo hakupigwa risasi, ka mujihu wa msemaji wa polisi mjini Washington.
Alikamatwa na kisa hicho kikasababisha kufungwa kwa moja ya majengo ya bunge.
Kisa hicho kinajiri baada ya kushuhudiwa mashambulizi kadha ya kugonga kwa magari miji ya London na Brussels,
Msemaji wa polisi Eva Malecki, amesema kuwa mshukiwa ni mwanamke na kisa hicho ni cha uhalifu.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPolisi wakiweka ulinzi katika bunge la Marekani

Kisa hicho kilitokea wakati maafisa waligundua dereva ambaye alikuwa akiendesha gari kwa njia isiyo ya kawaida na kutaka kumsimamisha.
Dereva huyo kisha akageuza gari kwa haraka na nusura awagonge polisi.
Sababaua ya kisa hicho haijulikani na mwanamke huyo hajatambuliwa.
Vikao vya bunge vinaendelea kama kawaida na watalii wameruhusiwa kurudi eneo hilo.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.