Na Yusuph Mwamba
UCHUNGUZI uliofanywa na Samsung kuhusu visa vya simu aina ya Galaxy Note 7 kushika moto, umebaini kwamba visa hivyo vilitokana na kasoro kwenye betri.
Kampuni hiyo iliacha kutengeneza na kuuza simu hizo Oktoba mwaka jana baada ya visa hivyo kuripotiwa kwa wingi.
Simu ambazo zilitolewa upya pia zilikuwa zinashika moto.
Lakini Jumatatu, Samsung imesema tatizo halikutokana na programu za simu hiyo iliyotarajiwa kutoa ushindani kwa simu za iPhone zinazotengenezwa na kampuni ya Apple.
Hatua ya kuzichukua tena simu zote zilizokuwa zimeuzwa inakadiriwa kuigharimu kampuni hiyo ya Korea Kusini jumla ya $5.3bn (£4.3bn) na kuathiri pakubwa sifa za kampuni hiyo.
Uchunguzi wa ndani na uchunguzi huru "umebaini kwamba betri ndizo zilizokuwa chanzo cha moto katika Note 7," Samsung imesema kwenye taarifa.
Kampuni hiyo imesema kasoro kwenye uchoraji wa muundo wa betri hizo pamoja na kasoro kwenye mfumo wa utengenezaji wa betri hizo, zilisababisha betri hizo ambazo ziliundwa na kampuni mbili kuwa na kasoro.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi, matatizo yanatokana na betri hizo kuwa kubwa na hivyo kutotoshea vyema kwenye sehemu yake ndani ya simu.
Aidha, hakukuwa na nyenzo za kutosha za kukinga betri hizo dhidi ya joto.
Samsung imesema inawajibika kutokana na "kukosa kwetu kutambua na kuthibitisha matatizo yaliyotokana na muundo wa betri na kasoro kwenye uundaji wa betri."
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment