Na Issa Ramadhani
ADHABU ya kifo nimauaji ya mwanadamu yanayotekelezwa na serikali baada ya mahakama kutoa hukumu ya mauti kulingana na sheria za nchi.
Kwa kawaida adhabu hiyo inatolewa kwa jinai nzito sana, lakini kubwa zaidi ni hili lililotokea nchini Kenya baada ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kutatilisha hukumu ya wafungwa zaidi ya elfu mbili ambao walikuwa wamehukumiwa kifo.
Rais amebadilisha hukumu hiyo na sasa wafungwa hao 2,747 watatumikia hukumu ya maisha jela.
Wahalifu wamekuwa wakihukumiwa kifo Kenya lakini hakuna aliyewahi kuuawa tangu miaka ya 1980.
Watetezi wa haki wamekuwa wakipigania kuondolewa kwa hukumu hiyo.
Baadhi ya wafungwa hata hivyo wamekuwa wakilalamika kwamba hakuna tofauti ya hukumu ya kifo na maisha jela kwani mfungwa huwa anaishi jela hadi kifo chake.
Rais Kenyatta pia amewaachilia huru wafungwa 102 waliokuwa wakitumikia vifungo virefu.
Alhamisi wiki iliyopita, Rais Kenyatta alikuwa amewaachilia huru wafungwa takriban 7,000 wa makosa madogo madogo au waliokuwa wanakaribia kumaliza kutumikia vifungo vyao, na ambao walikuwa wameonyesha dalili za kubadilisha tabia.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment