Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
AJALI (kutoka neno la Kiarabu) ni tukio maalumu linalotambulika na lisilotarajiwa, geni na lisilotakikana ambalo hutokea katika muda na mahali fulani bila sababu au makusudi dhahiri, lakini husababisha madhara yaliyo wazi, hasa vifo.

Ajali hudokeza kwa ujumla matokeo mabaya ambayo labda yangeweza kuepukwa au kukingwa ikiwa matukio yaliyosababisha ajali hiyo yangetambuliwa na kurekebishwa kabla ya tukio hilo.
Takwimu zinaonesha kuwa, nchi kama Malawi, Kenya, na Afrika kusini ndio nchi hatari zaidi kutembea kwa miguu na kuendesha baiskeli, utafiti wa Umoja wa mataifa kuhusu ajali za barabarani unasema.
Kati ya watu milioni 1.3 wanaofariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, 49% ni watu wanaotembea, waendesha baiskeli na pikipiki, shirika la mazingira la Umoja wa mataifa UNEP linasema.
Hizi ndizo takwimu za watu waliokufa wakitembea au wanapoendesha baiskeli katika ajali za barabarani:
  • Malawi: 49% wanaotembea, 14-17% wanaoendesha baiskeli
  • Kenya: 47% wanaotembea, 14% wanaoendesha baiskeli
  • Afrika kusini: 50% wanaotembea, 3% wanaoendesha baiskeli.
UNEP linasema uwekezaji wa dharura unahitajika kuimarisha miundo mbinu ya kutembea na kuendesha baiskeli ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.
Ripoti ya utafiti huo wa UNEP iliyopewa jina 'Global Outlook on Walking and Cycling', inaeleza kuwa ukosefu wa uwekezaji katika kuhakikisha watu wanatembea na kuendesha baiskeli salama ndiyo unaochangia vifo vya mamilioni ya watu na kupuuza nafasi nzuri ya kuchangia katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.