Halloween party ideas 2015
Image

na Issa Ramadhani.
TIMU ya soka ya Mbeya City imetoa onyo kwa Simba kuwa hawatatoka salama kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kesho, kwani wamejipanga kuifunga na kubakiza pointi tatu.
Msemaji wa Mbeya City, Dismas Ten aliliambia gazeti hili jana kuwa Simba isitegemee kushinda kwa urahisi kama ilivyofanya katika mechi zake zilizopita kwani hata wao wamejipanga na wanahitaji ushindi. Alisema wanaifahamu ni timu nzuri na wanawaheshimu, lakini ubora wao hauwaogopeshi katika kujituma na kupata ushindi.
“Simba wajiandae vya kutosha kwa sababu tumedhamiria kufunga magoli mengi, tunajua tabia zao wanapofungwa, lazima wakae,” alisema.


Ten alisema kinachohitajika ni waamuzi wachezeshe mchezo kwa kufuata sheria 17, ili mashabiki wapate burudani na kufurahia ushindi kwa timu yao.
Timu hiyo inajivunia kufikisha pointi 12 katika michezo minane iliyocheza hadi sasa ikishika nafasi ya nne, kwenye msimamo wa ligi.
Kwa upande wa Simba, huo utakuwa ni mchezo wake wa kwanza nje ya mkoa wake, ikitarajiwa kuendelea ushindi walioanza nao tangu kuanza kwa msimu na kutesa kileleni kwa pointi 17 katika michezo saba iliyocheza.


Msemaji huyo wa Mbeya City alisema wachezaji wake waliokuwa majeruhi Haruna Shamte na Sankhani Mkandawile wameanza mazoezi tayari kuivaa Simba kesho.
“Shamte na Mkandawile wamekuwa sehemu ya kikosi kilichofanya mazoezi jana hii ni tafsiri kuwa kikosi chetu kimetimia, Simba ni timu ambayo tunaijua, hatuna shaka nao mara kadhaa wamekuja hapa wakapata kipigo, tunafahamu wamekuwa na mwanzo mzuri wa msimu lakini kucheza na City ni jambo tofauti inawalazimu kujipanga sana, waje nasisi tupo tayari,” alisema.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.