MAADHIMISHO ya Saccos Duniani kote yakiwa yamefunguliwa rasmi,huku kitaifa yakifanyika Jijini Dar es salaaam Mnazi Mmoja ikiwa ni mfululizo wa siku
tatu kabla ya kuhitisha maadhimisho hayo, Serikali imesema itaendelea kushirikiana na vyama vya akiba na mikopo ili kujenga mazingira bora ya kuinua uchumi nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florens Turuka wakati wa ufunguzi wa Siku ya Saccos duniani uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florens Turuka wakati wa ufunguzi wa Siku ya Saccos duniani uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
“Vyama vya akiba na mikopo ni wadau wakubwa wa saccos Duniani kote yakiwa yamefunguliwai kwani vinasaidia sana katika kiinua uchumi wa nchi hivyo hatuna budi kuendelea kushirikiana” alisema Dk.Turuka.
Dk. Turuka aliwataka viongozi wa vyama hivyo kumaliza changamoto zao wao wenyewe na wanachama wao pale zinapotokea badala ya kukimbilia serikalini.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT), Benard Kalinga alisema vyama hivyo vimepata mafanikio makubwa kwani wamefanikiwa kuanzisha Saccos 4,000 ambazo zipo hadi vijijini na kuwa na wanachama milioni 1.5 nchini.
“Sheria namba sita ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013 imeanza kutumika baada ya kupata idhini ya Rais mwezi Oktoba 2013 lakini ni dhahiri kuwa kumekuwa na malalamiko mengi juu ya baadhi ya maeneo yaliyoko kwenye sheria hiyo” alisema Kalinga.
Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni cha Sanaa cha Magereza kikionesha umahiri wa kucheza ngoma aina ya chaso inayochezwa na wenyeji kutoka Pemba. |
Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni cha Sanaa cha Magereza kikitoa burudani kwenye hafla hiyo |
Baadhi ya wadau wakiwa kwenye maadhimisho hayo aliyeshika kipaza sauti ni Mc Mshana (katikati). |
Mjasiriamali Zamda Sasillo (kushoto), akiwa na wateja walitembelea banda lake katika maadhimisho hayo. Kutoka kulia ni Magdalena Samkumbi, Lubanzo Kalufya na Ashura Shoka. |
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), akizungumza na Ofisa Uendeshaji Mkuu, Mfuko wa Pembejeo, Pili Mogasa. |
Ofisa Masoko wa Benki ya Posta Tanzania, Ezekiel Fumbo (kushoto), akimuelekeza Dk. Turuka kazi mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo |
Ofisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo. |
Post a Comment