Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani
WADAU wa afya nchini, ikiwemo hospitali ya TMJ, wamezindua tovuti ya kwanza ya habari za ugonjwa wa figo inayotumia lugha ya kiswahili.
Katika tovuti hiyo iliyozinduliwa jana, Dar es Salaam kwa ufadhili wa TMJ, habari muhimu za kuzuia na kutibu matatizo ya figo yanayoongezeka barani Afrika ikiwemo Tanzania, zitapatikana kwa lugha hiyo ya taifa na kutoa mwongozo wa wagonjwa namna ya kuishi maisha salama.

Akizindua kitabu hicho, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwagwalla, alisema, “Upatikanaji wa kitabu cha figo na tovuti kwa kiswahili, kinachoongewa na watu wengi ni hatua kubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa ya figo. Hospitali ya TMJ na timu ya madaktari wamefanya kazi kubwa kwa ajili ya mradi huu kwa kuweza kuandaa kitabu cha figo na tovuti kwa wagonjwa wa figo kwa Kiswahili.”

Alisema kitabu na tovuti kuhusu ugonjwa wa figo kwa kiswahili vitawanufaisha mamilioni ya wagonjwa wa figo na takribani watumiaji wa kiswahili milioni 100 kupambana na ugonjwa wa figo.

Kigwangala alisema kwamba kitabu hicho kinalenga kutoa habari za msingi kwa wagonjwa na familia zao kuhusu matatizo yote ya figo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya TMJ, Dk Tayabal Jafferjie, alisema uzinduzi wa tovuti hiyo utawezesha Watanzania kupata taarifa mbalimbali sahihi kuhusu ugonjwa huo.

Kuhusu kitabu, Dk Jafferjie alisema kina kurasa 230 na kitawasaidia wagonjwa wa figo na watu wengine kufahamu afya yao ya figo na kuondoa mkanganyiko kuhusu matatizo yote ya figo. Dk Jafferjie alisema kwa wahitaji wa kitabu hicho wanaweza kukipakua bila malipo kutoka katika tovuti hiyo ya www.kidneyinSwahili.com
Kwa upande wake, Dk Gabriel Upunda, Mganga Mkuu wa Serikali mstaafu, alisema, “kupatikana kwa kitabu na tovuti hiyo itaongeza uelewa mpana kwa jamii ya Kitanzania, na hivyo kusaidia watu wengi kujilinda na madhara ya figo na mengine yanayofanana.
Kitabu na tovuti ya ugonjwa wa figo kwanza viliandaliwa kwa kiingereza na Dk Sanjay Pandya kutoka India huku kitabu na tovuti ya ugonjwa huo kwa kiswahili viliandaliwa na Dk Upanda.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.