TANZANIA ni nchi inayo ongozwa kwa misingi ya demokrasia na katiba, nchi yoyote ili iweze kusimama lazima iwe na katiba yake na wanachi pamoja na viongozi waitambue na kuilinda.
Katiba
ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania
SURA YA KWANZA
Sheria ya 1984 na.15.ibala .5
Sheria ya 1984 na.15.ibala .5
JAMHURI YA MUUNGANO,VYAMA VYA SIASA,WATU NA SIASA, YA UJAMAA NAKUJITEGEMEA
SEHEMU YA KWANZA
JAMHURI
YA MUUNGANO NA WATU
Kutangaza jamhuri yamuungano
Sheria ya 1984 Na.15 ibala.5.
1.Tanzania
ni nchi moja nan i Jamhuri ya muungano.
Eneo la Jamhuri ya muungano Sheia Ya 1984 Na.15 ibara 6.
2-(1) Eneo ia Jamhuri ya Muungano ni
eneo lote la Tanzania Zanzibar,na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapatikana nayo.
Sheria ya 1992 Na.4 ibala 4
(2)Kwa ajili ya
utekelezaji bora washughuli za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano au
serikali ya Mapinduzi,Rais anaweza
kuigawa Jamhuri ya muungano katika mikoa,wilaya na maeneo mengineyo,kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na sharia au mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Isipokuwa kwamba Rais atashauriana
kwanza na Rais wa Zanzibar kabla ya kuigwa TanzaniaZanzibar katika mikoa,wilaya
au maeneo mengineyo.
Tangazo la Nchi yenye mfumo wa vyama vingi Sheria ya 1992 Na.4 ib.5 Sheria ya 2005 Na.1 ib.4
3-(1)Jamhuri ya muungano ni nchi ya kidemokrasia na ujamaa
,isiyokuwa na dini,yenyekufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa
(2) Mambo yote
yahusuyo uandikishaji na uendeshaji wa
vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa
mujibu wa mashariti ya katiba hii na sharia iliyotungwa na bunge kwa ajili hiyo.
Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi Sheria ya 1984 na.15 ib.6 Sheria ya 2005 Na.1 ib.25
Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi Sheria ya 1984 na.15 ib.6 Sheria ya 2005 Na.1 ib.25
4-(1)Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika ya Muungano zitatelekezwa na
kudhibitiwa navyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji,vyombo viwili vyenye
mamlaka ya utekelezaji utoaji haki,na pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya
kutunga sharia na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma.
(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya Jamhuri ya muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilihi.
(3) Kwa ajli ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya kwanza iliyoko mwishoni mwa katiba hii, na pia kutakuwa na mambo yasiyo mambo ya Muungano .
(4) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti mengine yaliyomo katika katiba hii.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment