Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani

DUNIA kwa sasa ina maajabu mengi sana, hapa tunaangalia maajabu yatokanayo na afya, maajabu haya mara nyingi  kwa njia moja au nyingine yamekuwa ni yenye kushangaza na kusikitisha wakati mwingine.

Leo katika safu hii,utapata kumfahamu binti wa miaka 18,ambaye amezaliwa akiwa na tatizo la ngozi linalopelekea kutokuota nywele kinywani, huku ngozi yake ikiwa nene na ngumu yenye vigamba vidogo vidogo.

Inaelezwa kuwa, inaeleza kuwa binti huyo anayefahamika  kwa jina la  Hunter Steinititz,hawezi kufumba macho kutokana na tatizo hilo la ngozi linalosumbua.
Aidha, muonekano wa ngozi ya Hunter, unafanana na ngozi ya mtu aliyewahi kuungua na moto.
Mwana dada Hunter, akiwa pamoja na baba yake 

Wataalamu wa afya wameeleza kuwa, Hunter alikuwa na tatizo la jenetiki (genetic), ambayo kitaaluma huitwa harlequin ichthyosis, ambalo linasababisha seli za ngozi  kutokuwa na mafuta au unyevu (fatty moisture).

Licha ya ngozi kutokuwa na mafuta au unyevu, pia tatizo hili hufanya ngozi kuwa nene kupita kiasi huku ikiwa kavu sana, na kutokuwa na uwezo wa kutoa taka mwili ( kutokwa jasho) hata kama msichana huyo atafanya mazoezi au kukaa kwenye mazoezi au kukaa kwenye joto kali.

Hunter hulazimika kuvaa wigi kila siku, kwani kichwa chake hakina nywele kabisa.Wataalamu wa afya walieleza kuwa , follicles za nywele zimezibwa na ngozi, hali inayopelekea nywele kutokuota.

Aidha, tatizo hilo la ngozi linapelekea baadhi ya viungo vya Hunter kama vile vidole kutokuwa na mjongeo au kutonyumbuka.

"Sijawahi kutokwa jasho, kufumba macho wala kuota nywele, kutokana na tatizo hili linalonisumbua". Alisema Hunter

Watafiti wa masuala ya afya walieleza kuwa, tatizo hili ni nadra sana kutoke.Zamani watoto waliozaliwa na tatizo hilo huwa hawaishi zaidi ya mwaka mmoja kutokana na kukosa mafuta (fats) muhimu, ambayo hutoa kinga dhidi ya bakteria hatari ama maambukizi mengine.

Kw mujibu wa wataalamu hao, siku hizi tatizo hilo linaweza kudhibitiwa ili muhusika aweze kuishi miaka mingi zaidi ingawa bado hakuna tiba ya kuponesha kabisa.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline





Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.