MCHEZO wa mpira wa miguu, ni mchezo unaopendwa sana na watu takribani Ulimwengu mzima, katika mchezo huu mategemeo ya wengi ni kuona wanapata furaha na furaha hiyo huja na matokeo makuu matatu, yaani kushinda, kufungwa na kusuluhu.
Tumekuwa tukishuhudia matukio mengi sana katika katika mchezo huu, kwanza vituko vikubwa ni kuhusu ushangiiaji kuanzia kwa wachezaji na washangiliaji pamoja na mbwembwe za makocha hapo ndipo radha ya mpira hupatikana.
Hapa tunamzungumzia Nyota wa Kimataifa wa Morocco, Hicham Zerouali, nyota huyu alizaliwa mwaka 1977, kutokana na vitimbwi vyake na jezi yake nyota huyu alijipatia umaarufu kwa kupewa jina la utani la "Zero"
Zero, ni mmoja wa nyota nguli katika nafasi ya ushambuliaji, pia alishawahi kupata kutumikia vilabu mbali mbali kama vile Scotland, United Arab Emirates kote alikuwa akitumika katika nafasi ya ushambuliaji.
Zerouali, alifanikiwa kusaini katika klabu ya Aberdeen chini ya meneja Ebbe Skovdahl kutoka FUS de Rabat mwaka 1999.Licha ya kusakata kabumbu kwa kipaji cha hali ya juu na pia ndiye mchezaji pekee aliyewahi kuvaa jezi namba (0) katika mwaka 2000 na kuwa miongoni mwa wachezaji .waliowahi kufunga Hti triki katika klabu ya Dundee.
Zerouali alifunga Jumla ya magoli thelathiniwa katika raundi ya nne ya Scotland Cup mbali akiwa na klabu dhidi ya St Mirren huku wakifanikiwa kuchukua taji katika mechi ya marudiano.
Zerouali licha ya mafanikio hayo aliyoyapata lakini alifanikiwa kuifungia klabu yake goli katika ushindi wa magoli 2-0 mechi ya marudiano katika dimba la Pittodrie huku akiisaidia Aberdeen kuchukua ndoo katika raundi ya pili ya michuano hiyo katika kombe la scotland
Baada ya mkataba wake na klabu ya soka ya Aberdeen kumalizika, Zero, aliamua kuikacha klabu hiyo na kutimkia kunako Falme za kiarabu katika klabu ya Al- Nassr kwa muda wa mwaka mmoja na kurejea kuishi katika nchi yake ya Nyumbani ya Morocco mwaka 2003 na kusaini kunako klabu ya FAR Rabat na kufanikiwa kushinda Coupe du Trone mwaka huo huo.
Zerouali,miongoni mwa mafanikio aliyoyapata Nyota huyo ni pamoja na kushinda kofia 17, katika timu yake ya taifa ya soka ya Morocco na alifanikiwa kufumania nyavu mara tatu.
Pamoja na mafanikio hayo aliyoyapata , pia alifanikiwa kuchezea kunako Taifa lake la Morocco mwaka 2002 Kombe la Mataifa lililofanyika nchini Mali, naalifunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Burkina Faso . Pia Yeye pia alicheza katika michuano ya FIFA World Championship Vijana 1997. Alikuwa katika kikosi kimataifa mwezi mmoja kabla ya kifo chake.
Zerouali, aliuawa katika ajali ya gari Akiwa katika klabu yake ya Rabat mnamo Desemba 2004 huku akiwa na umri wa miaka miaka 27.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment