Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

FIGI FIGISU, si kwa Bongo tu, hata Ulaya zimeonekana kushika patamu, baada ya chombo kimoja cha habari kutoka Italia kuelezea huenda dili la mwanandinga wa kimataifa wa Ufaransa na Kiungo wa klabu ya Soka ya Juventus likakwama kutokana na ada ya uhamisho wa wakala wake.


Akizungumza na Sky Sports, mwanahabari ajulikanye kwa jina la  Valentina Fass amesema  kuwa pamoja na kuwa na majadiliano ya muda mrefu kai ya nyota wa Juventus  ,Paul Pogba , dhidi ya klabu ya soka ya Manchester United lakini bado majadiliano juu ya wakala wake yameonekana kuwa kikwazo juu ya malipo yake.


Pogba, ambaye tayari alishafanya mazungumzo ya awali na klabu ya Manchester United juu ya kurejea kunako klabu hiyo kaika dimba Old Trafford, ambapo yapita miaka minne tangu aondoke Manchester United na kujiunga na Juventus kwenye ligi ya  Serie A.
Licha ya  majadiliano na makubaliano binafsi yakiwa wamejadiliana na kuafikiana, lakini kazi inayoonekana kuwa ngumu ni  juu ya gharama za wakala wake mwanandinga huyo ,Mino Raiola, anayetaka kiasi cha Euro milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.
Kwa haili inavyozidi kuonekana, hii itamnyima raha meneja wa United, Jose Mourinho, aliyepanga kupata saini ya nyota wa nne katika kuijenga klabu hiyo kaitika msimu ujayo na kurejesha heshima iliyotoweka tangu kuondoka kwa aliyekuwa meneja wa zamani wa klabu ya United, Sir Alex Furguson.
Alikizungumza na chombo cha habari, mwandishi mmoja kutoka chombo cha habari cha Sky Spors ya Italia,Valentina Fass, amekuwa na haya yakuyazungumza;
 "Paul Pogba ,amekuwa katika mazungumzo mazuri na klabu ya Manchester United , walipofikia si pabaya sana, lakini katika makubaliano yao kati ya mchezaji na wakala pamoja na timu ndipo panapoweka ugumu wa nyota huyo kushindwa kusaini Manchester United" Alisema Valentina
" Katika moja ya makubaliano yao ni kwamba, katika mauzo ya nyota huyo, wakala atapata Euro milioni 20, huku Euro milioni 13 atapatiwa kama moja ya
pesa ya msimu wake wa usajili na Euro milioni 7 itakuwa ya haki ya matangazo yake, kitu ambacho kwa vilabu vyote kikionekana kuwa kigumu huku kila kilabu kikijitoa katika kujihusisha na malipo hayo" Aliongeza Mwandishi huyo.

Kwa sasa wakala huyo na mchezaji huyo wapo katika Jiji la Miami kwa ajili ya mapumziko mafupi ,kabla ya kurejea kunako klabu yake ya Juventus mwanzoni mwa mwezi Augusti.

Safari ya Raiola  kuelekea Jiji la Miami na nyota huyo, ilikuwa ni kwenda kuchambua vitu vya msingi ikiwemo pamoja na ada ya uhamisho wa mwanandinga huyo pamoja na pesa yake ya uhamisho kama wakala wa nyota huyo alioitaka.
Tatizo kubwa lililopo kwa sasa ni kiasi cha pesa anachokitakwa wakala wa mchezaji huyo baada ya vilabu vyote kuonekana kususia gharama hizo wakisema ipo juu sana huku Manchester United wakisema kama watalipa Euro milioni 110 hawatakuwa na pesa yakumpa wakala huyo kitu amabcho kinaonekana kuwa tatizo.
Mpaka sasa Meneja Jose Mourinho, ameshafanya usajili wa nyota watatu katika kampeni ya kujiandaa na msimu wa 2016/2017, baadhi ya nyota hao ni pamoja na  Eric Bailly kutoka Villarreal, Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na Kiungo wa klabu ya soka ya Borussia Dortmund  Henrikh Mkhitaryan.
Wakati  mzozo huo ukiwa unaendelea, Mourinho amepanga kuja na mfumo mpya kama watashindwa kumnasa nyota huyo basi watageuka kwa Nyota wa Paris St- Germain,  Blaise Matuidi .
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.