Halloween party ideas 2015
Image

MORINHO 'AFUNGUKA JUU YA KUONDOKA KWA RYAN GIGGS UNITED

Na Yusuph Mwamba

Hivi karibuni kumekuwepo na minong'ono mingi miongoni mwa midomo ya watu, huku kila mmoja akisema lake baada ya maamuzi aliyoyafikia mwanandinga wa kimataifa wa Scoland , Ryan Giggs , juu ya kutundika daluga lake kunako klabu ya Manchester United mwishoni mwa juma lililopita.
Ryan Gigg (kushoto) Clayton Blackmore (kulia) wakiwa pamoja Manchester United

Watu wengi hususani washabiki wa Manchester United, wameonekana kushtushwa na uamuzi uliochukuliwa na  mkongwe huyo aliyeitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka 29 na hatimaye kumaliza soka lake United akiwa kocha mchezaji baada ya kutimuliwa Davis Moyez huku akikabidhiwa nafasi ya kocha msaidizi akiwa chini ya Meneja aliyetimuliwa Lous Van Gaal.

Maneno mengi yalitupiwa kwa Meneja mpya wa klabu hiyo kwa sasa, Jose Morinho, wengi wo wamekuwa wakisikika wakisema  kuwa, Morinho ndiye amemfukuza Giggs baada ya ujio wake huku kila mtu akiwa anasema la kwake lakini mwisho ya yote Morinho amefunguka na kukisema kile kilicho mfukuzisha Giggs kunako klabu hiyo aliyodumu nayo kwa kipindi cha muda mrefu.

Leo ilikuwa ni siku ya kwanza kwa Morinho kuzungumza na vyombo vya habari tangu ateuliwe kuwa Meneja mpya wa klabu hiyo na haya ndiyo aliyoyazungumza kwenye mkutano huo.

"Namshukuru Mungu kunifikisha hapa, na pia shukrani ziende kwa viongozi wa klabu hii, Giggs ameitumikia klabu hii kwa muda mrefu sana, na hata ujio wangu tulimuahidi kumpa nafasi kubwa lakini hakubadili maamuzi yake, kipindi cha miaka 16 alisema anataka kuja kuwa kocha wa United lakini kwa mtazamo wangu Giggs hakuhitaji kuwa kocha msaidizi alihitaji kuwa kocha mkuu wa United, nilikuwa kocha msaidizi klabu ya Barcelona lakini niliamua kutafuta maisha pengine ulikuwa sio uamuzi rahisi lakini nilifanya napenda watu waamini mtu akiamua kufanya uamuzi anakuwa na lengo". Alisema Morinho


Aliongeza kuwa " kama Giggs atahitaji kurudi kunako klabu hii tutampokea kwa mikono yote, kwani mimi sina mamlaka ya kumzuia kwanza sijaja hapa kumfukuzisha mtu kazi nimekuja kwa maslahi ya United kuhakikisha inafikia malengo yake iliyojiwekea na kama Giggs atakuja kupewa klabu naimani atafanikiwa na atakuja kuwa kocha mkubwa sana Duniani kutokana na mafanikio yake ya soka aliyoyapata akiwa anasakata kabumbu" Aliongeza Morinho


"Manchester ni klabu kubwa Duniani, kwahiyo nimekuja kwenye klabu kubwa na historia yangu sifundishagi vilabu vidogo kutokana na mafanikio yangu mfano AS Roma, Inter-Milan, Chelsea pamoja na Real Madrid hapo utaona jinsi nilivyokuwa na mafanikio"




Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.