Na Yusuph Mwamba
MENEJA mpya wa klabu ya soka ya Manchester United, Jose Morinho, amemkabidhi mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza, Wayne Rooney nafasi ya ushambuliaji badala ya ya ile aliyokuwa akiitumikia awali chini ya kocha aliyefukuzwa Lous Van Gaal.
Morinho mwenye umri wa kiaka 53, ametoa maamuzi hayo mbele ya waandishi wa habari ikiwa ni mkutano wake wa kwanza akiwa kocha mkuu wa klabu hiyo.
Awali kabla ya ujio wa Jose Morinho, Wayne Rooney alikuwa akitumika kama kiungo mshambuliaji ambapo alikuwa akicheza namba 8 kwa 6, lakini ujio wa Morinho iumeonekana kuibadili safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo ambayo ilikuwa ikioongozwa na Dan Welback pamoja na kinda wa kimataifa wa Uingereza Marcus Rashdof.
![]() |
Morinho, akitoka kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu awe bosi mpya wa Manchester United leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo |
Uchezaji wa Rooney, akiwa kama kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo, kuliwafanya washabiki wa klabu ya United kuamini kwamba wamempata mrithi sahihi wa mwanandinga wa zamani Paul Scholes, ambaye alishatundika daluga kunako klabu hiyo.
![]() |
Wayne Rooney, akisalimiana na kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza, Roy Hodgson ,kwenye moja ya kombe la Euro 2016 Ufaransa |
"Wayne Rooney ni mzuri kwenye nafasi ya kiungo mshambuliaji, lakini kwa mimi sitotegemea Rooney acheze namba 8 au 6 nahitaji ,Rooney acheze safu ya ushambuliaji kwa kuwa ni mchezaji mzuri mwenye jicho la kuona goli, na katika dunia hii wachezaji wanabadilika kutokana na umri sasa, basi inakuwa ni mara chache kumbadilisha mchezaji na kuwa unavyotaka hicho kitu ni kigumu lakini kwa mimi na uzoefu huo basi nitafanya kazi yangu ipasavyo". Alisema Morinho
Ameongeza kuwa , ujio wake Manchester United ni kwa ajili ya kuifanya timu ishinde, wacheze vizuri pamoja na kuhakikisha United inafanikiwa kuwa miongoni mwa timu zitakazo fika katika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la mabingwa barani Ulaya maarufu kama Uefa Champions League mwaka 2017.
Wakati huo habari ya Rooney ikiendelea, lakini Manchester United bado ipo kwenye mawindo ya kumuwinda mwananndinga wa kimataifa wa Ufaransa ,Paul Pogba , ambaye alifanikiwa kuichezea kunako klabu hiyo kabla ya kutimka mwaka 2012 kwa kile kilicho daiwa kudharau klabu na utovu wa nidhamu ambapo United ilikuwa chini ya Sir Alex Furgason.
Kwa ada ya uhamisho wa Poga kama Manchester United itakuwa na nia thabiti ya kumuhitaji itawajibika kutoa kitita cha pauni milioni 80 katiak kupata saini ya Mwanandinga huyo ambaye anakipiga kunako klabu yake ya Inter-Milan ya Italia Serie A.
Post a Comment