Halloween party ideas 2015
Image

AZAM FC ' YALETA GOLIKIPA MZUNGU

Na Yusuph Mwamba

WAUZA RAMBA RAMBA wa klabu ya soka ya Azam FC, imemleta golikipa mzungu kutoka nchini Hispainia, Juan Jesus Hernandez, kwa ajili ya majaribio ya kuitumikia kunako klabu hiyo yenye maskani yake Chamanzi.

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa klabu hiyo, Jaffari Idd Maganga, amethibitisha ujio wa mwanandinga huyo na kusema kuwa yupo katika majaribio na kama atafanikiwa kufuzu basi atajiunga na klabu hiyo.

Licha ya msemaji kuthibitisha, naye kocha mkuu wa klabu hiyo raia wa Hispainia , Zeben Herndez, amesema klabu ya Azam kuna upungufu wa makipia kwa hiyo ujio wa Jesus, ni moja ya mikakati ya kuboresha safu ya langoni na kuifanya kuwa imara zaidi japo zipo nafasi nnyingine za kuzifanyia kazi.

Azam Fc inakuwa ni mara ya pili kumsjili mzunguu ,baada ya awali kumsajili Golikipa Obren Circovic mwaka 2011 akitokea kunako mabingwa wa ligi kuu msimu wa mwaka 2015/2016 klabu ya Dar Young Africans baada ya kutemwa kwa golikipa huyo.
Golikipa mpya wa Azam FC, Jesus Hernandez kutoka Hispain akiwasili uwanja wa Ndege Jk Nyerere  leo

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.