MWANANDINGA wa kimataifa Senegal anakipiga kunako klabu ya Shanghai Shenhua ya China Demba BA, watu wengi baada ya tukio la kuvunjika mguu
kutokea walitarajia huenda mwanandinga huyo akatangaza kutundika Daluga na maswala ya soka mapema kutokana na kuvunjika mguu wake wa kushoto, lakini mwenyewe amekanusha baada ya kufunguka kwa kusema bado mapema na anaimani atarudi Dimbani.
Ba mwenye umri wa miaka 31, mbaye alivunjika sehemu mbaya ya mguu wake wa kushoto, mpaka sasa hajafanyiwa upasuaji kamili kutokana na yeye mwenyewe kutaka kwenda Ulaya kwa ajili ya matibabu.
“Sikuwa nimewaruhusu wanifanyie upasuaji kamili kwa sababu nilitaka kwenda Ulaya kutibiwa lakini kutokana na hali yangu haiwezekani hivyo doctor atakuja hapa akitokea Ulaya, kiukweli sina mpango wa kustaafu mapema kwa sababu ya majeruhi yangu, kwani nimeona Hatem Ben Arfa akipata majeraha ya namna hii lakini alifanikiwa kurudi Dimbani na kuendelea na maisha ya Soka".Alisema Ba
“Hata ukiangalia Jeraha langu la mguu utaona kabisa halina utofayti na Hatem Ben Arfa, Kwa sasa ni kumuimba mungu na kufanikisha kupata matibabu bora zaidi yatakayofnya nipone haraka na kumalizika kwa tatizo ili niweze kurudi uwanjani haraka, kwani msimu wa Ligi ya Chinaunatarajia kumalizika November na huku msimu nmpya msimu mpya utaanza March, hivyo nitajitahidi kuhakikisha narudi mapema uwanjani kabla ya kuanza kwa msimu ujao.”Aliongeza Demba Ba
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment