Halloween party ideas 2015
Image


Na Yusuph Mwamba
MENEJA mpya wa klabu ya Soka ya Manchester United, Jose Mouronho, amesema ujio wa Kocha mpya wa timu ya Taifa ya Uingereza,, Sam Allardyce utaleta changamoto katika ligi hiyo.
Taarifa za kusainishwa kwa kocha huyo kuiongoza timu ya Taifa ya Uingereza zimethibitishwa na mwenyekiti wa FA ,Greg Dyke, baaada ya awali kutoa mapendekezo ya kocha gani anafaa kuiongoza Uingreza na hatimaya Sam kuibuka kidedea na kukabidhiwa timu.
Mkutano wa kumchagua Sam kuinoa Uingereza ulifuatiwa na mkutano wa bodi ya FA ulifanyika leo asubuhi nje ya Uwanja wa Wembley amabpo waliopitisha majina hayo na kumpata kocha mkuu ni pamoja na  FA chief executive Martin Glenn, Mkurugenzi benchi la ufundi wa FA  Dan Ashworth and Makamu mwenyekiti wa FA  David Gill, ambao walipendekeza kuwa Allardyce ni mtu sahihi kwao 


Mourinho, ambaye amekabidhiwa mikoba ya kuinoa klabu ya Man United, amesema anaamini kuwa ,Sam Allardyce , ni mtu sahihi wa Kuongoza Taifa hilo na kinachotakiwa ni kumpa ushirikiano mkubwa ili aweze kufanikisha mipango yake na Taifa hilo huku akimnadi kuwa ni mtu mwenye uzoefu na ligi kuu Uingereza maarufu kama England Backlays Premier League (EPL)


Ujio wa kocha huyo wa Sunderland ,umetokana na kuachia ngazi kwa aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza, Roy Hodgson, kufuatia matokeo mabaya aliyoyapata katika michuano ya fainali ya kombe la Euro 2016 baada ya kutolewa na timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland kwa jumla ya magoli 2-1 katika hatua ya robo fainali Nchini Ufaransa.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wake huliofanyika huko  Shanghai, ambapo klabu yake ya  Manchester United imeweka kambi ya maandalizi ya ligi kuu, Mourinho, amesema kuwa ,kulingana na Taifa lake kumuamini basi anafikiri kumpa timu kubwa kama Uingereza ni sahihi na wala FA hawajafanya makosa.



"Nafikiri ni uamuzi sahihi kwa mtu sahihi, pia ni chaguo bora sana, kwahiyo anahitaji nguvu na sapoti kubwa kwa chama cha mpira wa miguu Uingereza FA, hivyo basi nafikiri atafanya vizuri sana kutokana na uzoefu wangu naona ni mtu bora katika Dunia ya leo na chaguo sahihi la Waingereza".Alisema Mourinho
"Nafikiri, Sam kamwe hakuwahi kupata nafasi kubwa sana lakini amekuwa mtu mwenye uzoefu wa hali ya juu katika ligi kuu ya Uingereza, lakini hukuwa bora, lakini kwa sasa kwa upande wangu nafikiri yupo tayari na ni muhamasishaji mzuri nafikiri anaweza kutengeneza timu bora yenye nidhamu ya mpira pamoja na kuwatengenezea wachezaji wake nidhamu ndani na nje ya uwanja naimani atakuwa bora zaidi"
Licha ya Mourinho kumwagia sifa kem kem kocha huyo lakini alienda mbali zaidi na kusema haya;
"Kwa upande wangu siyo kama rafiki yangu lakini kwa upande wangu kama Meneja wa Manchester United, kitu ambacho nataka kumuahidi yeye ni kumtengenezea wachezaji wazuri na kumpa sapoti kubwa na kuwafanya wachezaji wa Uingereza wawe na hali ya mchezo ili kumsaidia yeye huku akisema anatumaini atafanya vizuri kwa vile huu ndio wakati wake, tunasubiri Uingereza kuwa kama Ureno walivyofika fainali Euro 2016 ,kwa sababu tangu mwaka 1966 hadi leo ni muda marefu kwahiyo ni kocha mkubwa tumpe muda".Aliongeza Mourinho


Miongoni mwa timu alizowahi kuzifundisha kocha Sam ni pamoja na Blackburn 2008,,West Ham 2011,Newcastle,Bolton 1999,Notts County 1997,Blackpool 1994,Limerick 1991-92 na klabu ya soka ya Sunderland ambako yupo kwa sasa.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline




Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.