Halloween party ideas 2015
Image


Na Yusuph Mwamba.

IKIWA  nisikuchache tu zilizopita baada ya DC wa Wilaya ya Kinondon, Ally Salumu Hapi, kufanya ziara baadhi ya  Vituo vya afya ikiwemoemo Tandale na Uwanja wa Fisi, sasa ameamua kufunguka rasmi juu ya  kuweka wazi mipango yake baada ya kushuhudia changamoto kadha wa kadha akiwa katika ziara hiyo.
Hapi amekuwa kati ya miongoni mwa ma DC moja walio na nguvu kubwa haswa ukizingatia aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo, Paul Makonda,kupandishwa  cheo na kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na aliyafanya mazuri, kwahiyo kwa nafasi aliyonayo DC Hapi naye  ameamua kuendeleza  mazuri hayo na ameamua kuyatoa yale aliyoyapanga yafanyike baada ya ziara yake aliyoifanya hivi karibuni.




Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa mapaka sasa kuna baaddhi ya mambo aliyoyagundua katika ziara yake ni pamoja na ufinyu wa nafasi katika Vituo vya Afya, upungufu wa vyoo katika Vituo  vya Afya, upungufu wa watumishi, uchafu katika vituo hivyo pamoja na ubadhirifu wa mali za umma uliofanywa katika Hospitali ya Kigogo.



Hapi amesema suluhisho la matatizo hayo litapatikana kwa kuhakikisha msongamano wa wagonjwa unapungua katika Hospitali ya Mwananyamala, pamoja na kuandaa mpango wa kujenga majengo mengine makubwa, kutenga sehemu za kuchomea  takataka kwa kununua mashine kubwa pamoja na kutoa motisha kwa wafanyakazi wataokuwa wanafanya kazi kwa juhudi kila baada ya miezi mitatu.



JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.