Nyota wa muziki Rihanna amejitolea
kufadhili elimu ya wanafunzi kupitia wakfu wake.
Hatua hiyo inaamanisha kwamba
watu kutoka jamii zisizojiweza watapata msaada wa kulipa ada ya shule.
Wakfu huo wa Clara Lionel umekuwa
ukifanya kazi tangu 2012 ambapo hutoa ruzuku kwa shule huko Barbados mbali na
kuwasaidia wagonjwa wa saratani.
Bibiye Rihana alifariki kutokana na ugonjwa wa saratani
mwaka huo huo na hivyobasi kumfanya yeye kuanza kusaidia sekta ya matibabu.
Kwa sasa shirika hilo limepanuka na kutoa ufadhili wa elimu
hadi kufikia dola 50,000 kwa wanafunzi waliopo
Barbados,Brazil,Cuba,Haiti,Guyana,Jamaica na Marekani. Sidhani
kwamba ni haki kwa watoto kubeba mzigo wa kifedha katika miaka walio
nayo'',alisema Rihanna
Post a Comment