Polisi nchini Uingereza
imethibitisha kuwa kitu kilichokuwa kinadhaniwa kuwa ni bomu
kilichoonekana kwenye uwanja wa timu ya Manchester United wa Old
Trafford hakikuwa bomu kama ilivyodhaniwa bali kilikuwa ni kifaa cha
wanausalama cha mazoezi kwa ajili milipuko.
Kifaa hicho kiliachwa
na walinzi wa kampuni moja ya binafsi baada ya kufanya mazoezi
yaliyowahusisha mbwa wenye kunusa vifaa na vitu vya kihalifu.
Kutokana na kuonekana kwa kifaa hicho mechi kati ya Manchester United na Bournemouth iliahirishwa.
Tayari kifaa hicho kimeshaharibiwa chini ya uangalizi mkali wa timu ya kuthibiti milipuko.
Tayari maafisa wa mji wametaka uchunguzi ufanyike na kuita kitendo hicho kuwa ni cha kizembe na cha kudhalilisha.
Maelfu
ya mashabiki walioondolewa katika uwanja wa Old Trafford ambapo mechi
baina ya wenyeji Machester United na Bournemouth iliahirishwa na
itachezwa siku ya jumanne.
Post a Comment