Halloween party ideas 2015
Image




Mwigizaji wa filamu  za bongo, Jacqueline Wolper amesema sababu iliyomfanya apunguze kuvaa nguo za kiume ni  mahusiano mchumba wake aliyekuwanae sasa hapendelei akimuona amevaa nguo za kiume.
Mwigizaji uyo anaependwa na watu wengi alishawahi kupata skendo ya kufanya mapenzi ya jinsia moja (usagaji)japo yeye mwenyewe amekanusha habari hizo kuwa si za kweli.
Akiongea kwenye kipindi cha Nirvana kinachoruka EATV Wolper amesema nilikuwa navaa vile kwa wakati ule lakini kwa sasa mi nina mchumba   
“Nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule ulivyokuwa. Kuna watu walikuwa wanapenda, lakini sasa hivi nimeshakuwa mchumba wa mtu. Ni kweli lazima nivae gauni, kwahiyo mtu unatakiwa ujibadilishe wewe mwenyewe usisubiri kubadilishwa,” aliongezea.
Pia Wolper alisema, “hata hivyo bado sijaacha kabisa, kidogo unakuwa unagusia mashabiki zako wanakuwa wanakupenda.”

Hata hivyo Wolper japo amekiri kuwa na mchumba mpya kwa sasa lakini hayupo tayari kuweka mahusiano yake hadharani kama mwanzo alivyokuwa anafanya.

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.