Raisi John Magufuli
ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Kituo cha uwekezaji (TIC) Julietth Kairuki kuanzia tar 24 aprili
2016 baada ya kupata wasiwasi na muenendo wake wa kutochukua mshahara wa
serikali kwa muda wa takribani miaka 2.
Hatua hiyo imefikiwa baada
ya mheshimiwa raisi kupata taarifa kwamba mkurugenzi huyo amekuwa akiacha
mshahara wa serikali tangu alipopata ajira mnamo mwezi Aprili 2013 jambo ambalo
limezua maswali mengi.
Aidha mchakato wakupata
mkurugenzi mpya unaanza ambapo katika
kipindi hiki nafasi ya mkurugenzi mtendaji itasimamiwa na Clifford Katondo
Tandari.
Mwaka 2013 Bi Julieth
Kairuki aligoma kupokea mshahara uliopangwa na serikali akitaka mshahara mkubwa
zaidi pia alituhumiwa kusafiri hovyo nje ya nchi akijihidhinishia posho
kubwa zinazozidi mshahara wake. Pia
alikuwa na mahusiano mabaya ya kiutendaji na baadhi ya wafanyakazi.
Ni juzi tu Raisi Magufuli alivunja bodi ya mamlaka ya
mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo
Dr Hali Yahya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo mkataba wa utekelezaji wa
mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza
ya takribani sh bilioni 400 kwa mwaka
Post a Comment