Msanii mkongwe wa muziki, TID amesema kipindi cha nyuma alikuwa
anatoka kimapenzi na malkia wa filamu Wema Sepetu lakini baadae alitemwa hali
ambayo ilimuumiza sana.
kizungumza katika kipindi cha Clouds TV Ijumaa hii, TID amesema
hali hiyo ilimfanya atoke na wasichana wengi.
“Nilikuwa ‘namdate’ Wema Sepetu akaniambia sikutaaki, tangu
kipindi hicho nimekuwa na wasichana wengi. Ikitokea Wema anataka kurudi hakuna
nafasi, I’m occupied,” alisema TID.
TID amesema katika kipindi hicho aliumizwa sana na jinsi
magazeti yalivyokuwa yanamuandika vibaya.
“Wakati huo mitandao ya kijamii haikuwepo lakini wamagazeti
walizichukua picha na kufanya yao, it was bad. Mimi nikasema sawa lakini
niliumia sana,” alisema TID.
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya
‘Confidence’ aliyomshirikisha Joh Makini pamoja na
Dully Sykes.
Post a Comment