Miongoni mwa vitendo vinavyochangia uharibifu mkubwa wa mazingira nchini ni ukataji miti kwa ajili ya kilimo, nishati ya mkaa na kuni Hali kadhalika utengenezaji wa fanicha.
Vitendo hivyo vya ukataji wa miti bila kibali maalumu vimedhidi kukithiri siku hadi siku huku serikali ya tanzania ikiendelea kukemea vikali uharibifu huo wa mazingira kwa ukataji wa miti, pamoja na kuwafungulia mashitaka wale wote wanaojihusisha na ukataji wa miti bila kibali maalum.
Hali hiyo imepelekea Mkuu wa wilaya Temeke felix Lyaniva kumpa siku tatu mwenyekiti wa Mwenyekiti wa mtaa wa msakala kata yombo makangalawe Bw Denis Moyo kujisalimisha katika kituo cha polisi mara baada ya tuhuma za kuruhusu kukatwa miti hiyo.
Agizo hizo la Mkuu wa wilaya Temeke Dsm, Felix Lyaniva limekuja kufuatia kuhusika na ufyekaji wa msitu wa Serikali baada ya kukamata magogo ya miti iliyokatwa katika bonde la msakala wilyani humo kwa idhini ya mtendaji wa mtaa na Mwenyekiti wa mtaa wa msakala jambo ambalo linadaiwa kuwa kinyume cha sheria.
DC Lyaniva ameeleza kuwa mpaka sasa anashikiliwa mtendaji wa kata hiyo, na Kwamba wamepokea taarifa kuwa Mwenyekiti wa mtaa huo Denis Moyo amekimbia na hivyo amempa siku mbili ajisalimishe mwenyewe kwenye kituo cha Polisi Cha Temeke.
Kwamujibu wa mkazi wa eneo hilo Mohamed Mmeya amemueleza DC Lyaniva kuwa walipojaribu kufuatilia kwa watu waliokuwa wakikata miti hiyo walijibiwa kuwa viongozi hao wa Serikali ndio waliotoa vibali vya kuvuna miti hiyo.
Kwa upande wake mkuu wa kituo cha Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke SSCP Muhudhwar Msuya amethibitisha kuwashikilia watu 10 akiwemo mwanamke mmoja katika tukio hilo, na kwamba wamewakuta na mashine moja ya kuchania magogo na kwamba wanaendelea na upelelezi na mahojiano.

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Felix Lyaniva akiongea na wananchi waliokumbwa na adha ya ukataji wa miti. |
Hali hiyo imepelekea Mkuu wa wilaya Temeke felix Lyaniva kumpa siku tatu mwenyekiti wa Mwenyekiti wa mtaa wa msakala kata yombo makangalawe Bw Denis Moyo kujisalimisha katika kituo cha polisi mara baada ya tuhuma za kuruhusu kukatwa miti hiyo.
Agizo hizo la Mkuu wa wilaya Temeke Dsm, Felix Lyaniva limekuja kufuatia kuhusika na ufyekaji wa msitu wa Serikali baada ya kukamata magogo ya miti iliyokatwa katika bonde la msakala wilyani humo kwa idhini ya mtendaji wa mtaa na Mwenyekiti wa mtaa wa msakala jambo ambalo linadaiwa kuwa kinyume cha sheria.
DC Lyaniva ameeleza kuwa mpaka sasa anashikiliwa mtendaji wa kata hiyo, na Kwamba wamepokea taarifa kuwa Mwenyekiti wa mtaa huo Denis Moyo amekimbia na hivyo amempa siku mbili ajisalimishe mwenyewe kwenye kituo cha Polisi Cha Temeke.
Watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la ukataji wa miti bila kibali maalumu wakiwa chini ya ulinzi wa polis katika kituo cha polisi cha chang"ombe jijini Dar es salaam |

Post a Comment