Halloween party ideas 2015
Image

Na Mwandishi wetu

IDADI  ya watu waliopoteza maisha kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, imeongezeka na kufikia zaidi ya watu mia tatu.
Inaofiwa kwamba miili zaidi iko chini ya vifusi.
Jitihada za kuokoa zilisitishwa kwa muda baada ya giza kuingia.

Madhara yaliyosababishwa na mvua nyingi
Rais Ernest Bai Koroma amesema kupitia televisheni kwamba vituo vya dharura vimewekwa ili kukabiliana na kile alichokiita janga la taifa.
 Maporomoko ya udongo

Shirika la Msabala mwekundu limesema inakadiriwa zaidi ya watu laki tatu wamepoteza makazi yao.
Eneo lililoathirika zaidi wilaya ya Regent iliyopo pembezoni mwa mji wa Freetown baada ya mlima uliojaa maji kuporomoka.

 IUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, 
insta@wabunifumediaonline
.

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.