Na Mwandishi wetu
BAADA ya zile taarifa kuwa Juuko Murshid anatarajia kutua Yanga, Simba wameamua kumshusha jijini Dar es Salaam.
Juuko
raia wa Uganda ametua jijini Dar es Salaam na moja kwa moja amekwenda
katika ofisi za mmoja wa wafadhili wa Simba, Mohammed Dewji.
Dewji maarufu kama Mo, ameonekana akiwa na Juuko pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe.
Kitendo
cha Juuko kuonekana akiwa na Mo na Hans Poppe, imekuwa ni faraja kubwa
kwa Wanasimba ambao wameanza kuwazodoa watani wao Yanga.
Hata
hivyo, imeelezwa Juuko alikuwa na mpango wa kujiunga na Orlando Pirates
ambayo itafunishwa na Sredojevic Milutin ‘Micho’ raia wa Serbia
aliyekuwa akiinoa timu ya taifa ya Uganda.
IUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline .
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline .
Post a Comment