Na Yusuph Mwamba
RAIS wa Marekania Donald Trump anatarajiwa kufanya ziara nchini Uingereza mwaka ujao.
Bwana
Trump alikubali mwaliko wa Malkia wa kumuomba afanye ziara nchini
Uingereza wakati waziri mkuu Theresa May alifanya ziara nchini Marekani
mwezi Januari.Lakini ziara hiyo ilizua utata na hadi hata kusababisha Trump kubadili fikra zake.
Inaripotiwa kuwa hakutaka kuifanya ziara hiyo wakati kuna upinzani dhidi yake.
- Watu milioni moja hawamtaki Trump Uingereza
- Wanaharakati wataka Trump asizuru Uingereza
- Spika akataa Trump kuhutubia bunge Uingereza
- Trump amteua tajiri kuwa balozi Uingereza
Wanasiasa wakuu akiwemo kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn, na aliyekuwa kiongozi wa chama cha Lib Dem Tim Farron walitaka ziara hiyo kufutwa.
Maswali yaliibuka kuhusu ni kwa nini Trump alialikwa muda mfupi baada ya kuingia ofisini.
IUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment