Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, amewataka askari polisi wanawake kutoka kwenye Shirikisho la Majeshi la Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) washiriki kikamilifu katika oparesheni mbalimbali ambazo zinafanyika kwenye ukanda huo kama hatua ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku Tatu ya Polisi wanawake kutoka nchi wanachama wa SARPCCO katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais pia amewahimiza askari polisi wanawake kufanya kazi kwa bidii na kujituma hatua ambayo itasaidia kupanda vyeo kama askari wanaume katika maeneo yao ya kazi, na kusisitiza kuwa muda wa kulalamika kuwa hawapandishwi vyeo umeshapitwa na wakati bali kwa sasa wachape kazi na waonyeshe kuwa wanaweza majukumu yao wanayopangiwa ili waweze kupanda vyeo."Vyeo haviji tu ni lazima polisi wanawake muonyeshe kuwa mnaweza ili muweze kupandishwa vyeo na kupata nafasi za uongozi katika Majeshi yenu"
Kuhusu utendaji kazi wa Polisi wanawake, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka polisi hao kutumia mkutano huo wa siku Tatu kujadili kwa kina namna ya kuondoa changamoto hizo zinazorudisha nyuma utendaji wao wa kazi.

Amesema kama polisi wanawake wataacha majungu na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwao watafikia malengo yao haraka hasa katika kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo biashara ya dawa za kulevya.Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema anaimani kubwa kuwa mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa polisi hao wanawake kuimarika ipasavyo katika utendaji wao wa kazi.

Masauni pia amewahimiza polisi wanawake wanaopata mafunzo hayo kwenda kuwaelimisha na wenzao mipango na mikakati waliyoweka katika kulinda raia na mali zao katika nchi zao.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.