Halloween party ideas 2015
Image






NA JOHN SIMWANZA

Muasisi na Mtayarishaji wa Muziki wa kizazi kipya P Funk majani ambaye pia ndio mmiliki Halali wa Studio Ya Bongo Records  Ameamua kurudi Upya katika Uwanja huu wa Sanaa ya Muziki kitofauti kabisa baada Ya kuwa  mbali kidogo na Muziki kwa miaka Kadhaa iliyopita.

Ukizungumzia Wadau waliokua wanaupigania Muziki huu wa kizazi kipya Tangu Uanze Jina la P Funk lina nafasi kubwa sana naya aina yake Sio tu kwa Kutayarisha kazi kama Prudyuza Bali Majani Alikua anawasimamia wasanii wengi sana na kuhakikisha Wanafanya Muziki Ambao utawafanya Wapate Mashabiki watakao kuwa wanaunga mkono katika kununua kazi zao na pia kuhudhuria katika Show Mbali mbali zilizokua zina andaliwa zaidi na Wamiliki wa Kumbi za Starehe,Wamiliki wa Studio Pamoja na Mapromota kwa Wakati ule.

Ukaribu wa P funk Majani na Karabani Haujaaza hivi Karibuni kwani ni Miongoni mwa watu wake wa karibu sana Tangu Miaka ya 1999 Wakati wakati huo wakiwa na Kundi ambalo lilikuwa likitambulika kwa jina la 'NO NAMEZ' Kundi ambayo lilikua na linaundwa na Wasanii pamoja na Waandaaji wa Muziki na Karabani nae alikua  ni miongoni mwa wanakundi hilo la NO NAMEZ

Ujio wa Majani kwa kipindi hiki umekuwa ni ujio wa Kibiashara zaidi ya muziki kama Jinsi ambavyo Muziki umebadilika na kutoka kule ulikokua hauusishwi na biashara na kuja huku ambako Umekuwa niwabiashara zaidi na kuwa na Uwekezaji  mkubwa Ambao mara nyingi uwekezaji wake umekuwa na Matunda au Mafanikio makubwa.

Ukiachiliambali swala la Audio kwa sasa Kitu kinachokua katika Mawazo ya msanii na Mashabiki wengi ni Upande wa Video kwani kumekua na Ushindani mkubwa sana kiasi cha kufikia hatua ya Kuwafanya Wasanii wapunguze Safari Za kwenda nje kufanya Video na kupunguza swala la kumchukua Muongozaji wa nje kuja kufanya kazi Nchini kama ilivyokua kwa Godfather pamoja na Justin Cumpos hiyo hali inaashiria kuwa Muziki wetu umekuwa na Uwezo wa Waongozaji wa Video hizi umekuwa na Ubunifu mkubwa na wakisasa zaidi unaohitajika na wasanii katika Soko hili lenye Ushindani mkubwa kwa sasa.

Hakuna Alietegemea kama karabani Atarudi kwa Uwezo mkubwa kama Ule na Hakuna aliefikilia kama 'Wape' ya Bongolos itaongozwa na huyu Mwanaharakati na Miongoni mwa waasisi wa Mpira wa kikapu Nchini Tanzania Lakini Video kaitendea haki na Imekuwa yenye mapokeo makubwa na kuendana na Viwango vilevile vya Waongozaji wanao Tamba kwa sasa hapo ndipo huwa tunapokuja kutambua Maana ya msemo usemao 'Yakale ni Dhahabu' au 'Ng'ombe hazeeki maini'

Kutokana  na Karabani Kuitendea haki Wape ya Bongolo's iliyo chini ya P funk Majani Kunauwezekano Mkubwa pengine Ukawa ndio Ujio wake kwani Wasanii wengi watahitaji sana kufanya nae kazi kutokana na Uwezo alio nao ukilinganisha na Baadhi ya Video ambazo alisha wahi kuzifanya Wakati Ule kuwa Zina Utofauti Mkubwa Sana Na hii iliyo Muibua tena Kwenye Game ya sasa.

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.