Na Yusuph Mwamba
TIMU ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys, leo itapambana na Black Starlets ya Ghana kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Taifa,Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni, Serengeti Boys itautumia kama ni ishara ya kuwaaga mamilioni ya Watanzania kabla ya kusafiri kwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu.
Lakini kabla ya kutua Gabon, Serengeti Boys itakwenda Rabat, Morocco kufanya kambi ya takribani mwezi mmoja kuanzia Aprili 5, mwaka huu.
Ikiwa huko angalau itacheza mechi za kirafiki zisizopungua mbili dhidi ya wenyeji Morocco na timu nyingine ya jirani ama Tunisia au Misri. Kambi hiyo ya Morocco itamalizika Mei mosi, mwaka huu ambako timu itasafiri hadi Cameroon.
Ikiwa Cameroon, timu itacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya wenyeji yaani Mei 3 na 6, mwaka huu kabla ya kusafiri Mei 7, mwaka huu kwenda Gabon ambako Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola.
Vipimo vya mechi dhidi ya Ghana kadhalika hapo baadaye Cameroon, vitakuwa mwafaka kwenye kufanya tathmini ya uwezo wa Serengeti Boys kwani wapinzani hao wamekuwa na rekodi nzuri kwenye soka la vijana na kwa kipindi hiki zimepangwa kundi A pamoja na wenyeweji Gabon na Guinea
Mungu ibariki Serengeti Boys, Mungu ibariki Tanzania "Kutoka Gaboni mpaka kombe la Dunia".
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment