Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
MLINZI  wa zamani wa timu ya taifa ya England  na Aston Villa ,Ugo Ehiogu, amefariki dunia baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo Alhamisi.
Ehiogu, mwenye umri wa miaka 44, alipatwa na mshtuko wa moyo akiwa katika kituo cha mazoezi cha klabu ya Tottenham Hotspur
.
Taarifa ya Spurs ilsiema Ehiogu alifariki mapema Ijumaa akiwa hospitalini.
Ehiogu, ambaye alikuwa mkufunzi wa timu ya Spurs ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23, alikuwa alifanikiwa kuchezea kunako timu yake ya Taifa ya Uingereza katika jumla ya michezo minne  na kupachika bao moja.

"Hatuwezi kueleza majonzi na huzuni tuliyo nayo katika klabu hii," mkuu wa ukufunzi na ustawi wa wachezaji Tottenham John McDermott amesema.

Ehiogu aliwahi kuichezea kunako klabu ya soka ya  Aston Villa karibu mechi 200 kati ya 1991 na 2000 kisha akajiunga kunako klabu ya soka ya Middlesbrough kwa kandarasi ya miaka saba.


Ehiogu, Alishinda Kombe la Ligi akiwa na Villa mwaka 1994 na 1996 na pia akiwa na Boro mwaka 2004.

Beki huyo pia alichezea West Brom, Leeds, Rangers na Sheffield United, kabla ya kustaafu 2009.

Alianza kazi ya ukufunzi Tottenham mwaka 2014.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline



Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.