Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Kimatifa wa Brazil na aliyewahi kukipiga kunako klabu ya Real Madrid, Ronaldo Nazario de Lima, amemshauri Mbrazil mwenzake anayekipiga katika klabu ya Liverpool, Philippe Coutinho, kufuata nyayo zake na kuhamia katika dimba la Santiago Bernabeu.

Coutinho mwenye umri wa miaka 24, amekuwa na wakati mzuri ndani ya Liverpool ambapo alinyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo msimu uliopita kutokana na umuhimu wake mkubwa katika kikosi cha kocha wake



Kwa upande wake Ronaldo ana imani ya kumwona Coutinho akiikacha Liverpool na kutua Madri baada ya mkataba wake kumalizika mwaka 2020.

Ronaldo alisema hayo alipoulizwa ni mchezaji gani ambaye angependa kumuona akitua kwa miamba hao wa Ligi Kuu Hispania (La Liga).

“Natamani kumwona Coutinho akiwa Madrid,” Alisema Ronaldo.

Katika dirisha la usajili la msimu uliopita barani Ulaya, Coutinho alihusishwa kuhamia Bernabeu kutoka Liverpool ambayo ilimbeba kutokea Inter Milan.
Mpaka sasa kiungo huyo ameifungia Liverpool mabao matatu ndani ya mechi nane alizocheza kwenye Ligi Kuu ya England msimu huu.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.