Na Issa Ramadhani
MENEJA wa klabu ya soka ya Manchester City ,Pepe Guardiola, amesema kuwa hatobadili filisofia yake licha ya klabu yake kufungwa 4-0 na Barcelona katika uwanja wa Nou camp.
Lionel Messi alifunga hat-trick dhidi ya Manchester City iliokuwa na safu ya ulinzi ilio legea huku kipa Claudio Bravo akipewa kadi nyekundu kwa kushika mpira nje ya eneo hatari.hakutakuwa na mabadiliko.
''Hadi siku ya mwisho ya kazi yangu kama mkufunzi nitajaribu kucheza kwa uwezo wetu'',alisema.
Barcelona inaongoza kundi C na pointi tisa ,ikiwa mbele kwa pointi tano.
City ilikuwa nyuma kwa bao moja katika dakika za kwanza za kipindi cha pili wakati Bravo aliposhika mpira na bahati mbaya ukamuangukia Luis Suarez.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment