Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani

KUJITOLEA na kuisaidia jamii kwa wana Ulimbwende umekuwa kwa kasi baada ya aliyekuwa Miss Tanzania 2016, Diana Edward ametangaza vipaumbe vyake  kuwa ni kupinga ukeketaji, mila potofu na ndoa za utotoni hasa kwenye jamii za Kimasai na nyinginezo.

Mrembo huyo aliyetokea wilaya ya Kinondoni, Diana alitwaa taji la Miss Tanzania 2016, usiku wa kuamkia Jumapili kwenye Ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.


Diana,  alinyakua taji hilo na kujitwalia gari aina ya Toyota IST na kitita cha Sh4 milioni baada ya kuwashinda warembo wenzake 29 kutoka mikoa mbalimbali nchini waliokuwa wakichuana kuwania taji hilo.

Akizungumza baada ya kutwaa taji hilo, Diana alisema haikuwa kazi rahisi kwani ushindani ulikuwa mkali ni mapenzi ya Mungu kumpa nafasi hiyo.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.