Na Yusuph Mwamba
BAADA ya Serikali ya awamu ya tano ikiwa na kasi ya kuimarisha michezo hapa nchini,hatimaye nyasi bandia na vifaa vingine kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza vimewasili huku ujenzi huo ukitarajia kuanza rasmi leo, Jumatatu. Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chama Soka cha Mkoa wa Mwanza (MZFA), Jackson Songora, alithibitisha kuwasili kwa makontena mawili yenye vifaa hivyo vilivyowasili juzi, Jumamosi.
Aidha, Songora, alisema kuwa vifaa vilivyowasili ni pamoja na nyasi bandia, magoli makubwa na madogo, gundi, trekta (kifaa cha kusafishia uwanja), nyavu na uzio.
Hata hivyo, Songora alisema kuwa tayari mkandarasi amemthibitishia ujenzi kuanza rasmi Jumatatu na kwamba anaamini ujenzi huo utakamilika kwa muda mwafaka.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment