Na Yusuph Mwamba
WINGA wa Kimataifa wa Walesi na anayekipiga kunako klabu ya soka ya Real Madrid, Gareth Bale, amekubali kuongeza kandarasi yake ya miaka 6 ya kutumikia klabu yake hadi mwaka 2022.
Bale mchezaji wa zamani wa Southampton alijiunga na klabu hiyo akitokea Tottenham Hotspur mwaka 2013.
Tiyari ameisaidia Madrid kushinda vikombe vitano katika misimu mitatu ya nyuma ikiwemo ligi ya mabingwa Ulaya mara 2 huku akifunga magoli 62 katika michezo 135.
Viungo wawili wa timu hiyo Luka Modric na Toni Kroos nao pia walisaini mikataba mipya mwezi huu.
Mkataba wa Bale unatajwa kuwa wa Euro 600,000 kwa wiki huku baada ya makato ya kodi ikiwa Euro 350,000
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment